Nafasi Ya Matangazo

October 10, 2012


Nasseb Abdul maarufu  Diamond na Lina Sanga wakifurahia madhari ya Bonde la Ngorongoro lililopo kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), juzi ili kuhamasisha wananchi walipigie kura Bonde la Ngorongoro lishinde katika maajabu saba ya Afrika.
 ********
Mahmoud Ahmad Arusha
Vijana nchini wameshauriwa kuvipigia kura vivutio vitatu vya utalii vilivoainishwa hapa Tanzania iliviweze kuingia kwenye shindano la vivutio vya asili vya afrika kwani wao wananafasi ya kufanya hivyo kwa kuwa wanatumia mtandao kwenye shughuli zao nyingi za kila siku.

Kauli hiyo imetolewa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Abdull Naseeb almaarufu Diamond na Linah Sanga kwa nyakati tofauti wakati walipotembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro mwishoni mwa wiki na kutanabaisha kuwa watatumia nafasi yao kama wasanii kuwaomba vijana wenzao kuvipigia kura vivutio hivyo ikiwemo mbuga ya Serengeti,Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake Diamond alisema kuwa alikuwa akiwaona wanyama hao kupitia kwenye runinga lakini ameweza kuwaona kwa uhalisia hivyo na kubaliana kuwa sasa tubebe uzalendo kuweza kuvitangaza vivutio vyetu mahala popote ulimwenguni na kuwataka vijana na watanzania kuanza kupenda utamaduni wa kutembelea mbuga zetu kwani mbona wageni kutoka nje ya nchi wamekuwa wao wakitembelea vivutio hivyo sisi je alihoji Diamond.

Diamond alisema kuwa Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio ambavyo ni nadra kukuta sehemu nyingine duniani lakini sisi tumekuwa nyuma kuvitangaza na kuvitembelea huku ni kuwa watumwa wa wenzetu na kuwataka vijana na watanzania kwa ujumla kuweza kuweka uzalendo na kuacha kutizama kupitia Runigani vipindi vya wanyama na kwenda kutembela mbuga zetu popote zilipo hapa nchini.

Na kwa upande wake msanii Linah Sanga alisema kuwa yeye alikuwa hajawahi kuwaona kwa uhalisia Simba na wanyama wengine kwa ujumla lakini ameweza kuona wanyama hao na pia ameweza kuona Create jinsi ilivyo akiacha alivyoso ma shuleni kwa kweli ni madhari ya kuvutia na inafaa kuipigia kura ili iweze kuwemo kweny maajabu saba ya Afrika.

Linah alisema kuwa wao kama wasani watawaomba vijana wenzao popote hapa nchini kutumia muda wao wa ziada kutembelea mbuga zetu ilikuweza kuitangaza vivutio hivyo kwenye kaya zao ili nchi yetu iweze kupata pato kupitia utalii wa ndani na kuwataka watanzania kuvipigia vivutio vyetu ilikuweza kushinda na taifa kuweza kuingiza pato.

Nae Dkt Fransic Mumba kaimu mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro alisema kuwa ni bahati kwa watanzania kupata nafasi ya vivutio hivyo vitatu ikwemo Ngorongoro,Serengeti na Mlima Kilimanjaro kuweza kupigiwa kura iliviweze kuingia kwenye maajabu saba ya Afrika na kuwataka watanzania kuvipigia kura Vivutio hivyo.

Dkt.Mumba alisema kuwa anawaomba vijana wengi kuvipigia kura vivutio hivyo kwa kuwa wamekuwa mstari wa mbele kwenye matumizi ya mtandao hivyo wataweza kupiga kura kwa urahisi huku akitanabaisha jinsi ya upigaji wa kura hizo.
Posted by MROKI On Wednesday, October 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo