Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi
Malangali, iliyopo mkoani Iringa, Steven Mligo akitoa elimu kwa watoto wenzake
juu ya Usalama barabarani na namna mbalimbali za matumizi sahihi ya barabara
ikiwa ni pamoja na kutambua alama mbalimbali za barabarani. Mligo alikuwa
akitoa elimu hiyo katika banda la Polisi Trafiki lililopo katika maonesho ya
Wiki ya Nenda kwa Usalma Kitaifa inayofanyika Mkoani Iringa katika uwanja wa
Samora chinbi ya Udhamini wa Kampuni ya simu ya Airtel.
Steven Mligo
akitoa mafunzo kwa watoto wenzake na kuonesha dhahiri uwezo wake na jinsi
alivyopata elimu hiyo ya usalama barabarani baada ya kupatiwa mafunzo shuleni
kwao na maofisa wa Trafiki.
Mtaalam wa
Elimu kutoka Mfuko wa Elimu Manispaa ya Iringa, Germana Kapinga (kulia)
akimsikiliza mkazi wa mjini Iringa aliyetembelea banda lao lililopo katika
maonesho ya Wiki ya nenda kwa Usalama viwanja vya Samora mjini Iringa leo.
Wakazi wa
mjini Iringa wakiwa katika banda la ASAS wakijipatia bidhaa mbalimbali
zitokanazo na maziwa.
Wakazi wa
mjini Iringa wakimsikiliza, Mwenyekiti wa Taasisi ya Usalama barabarani watu
wenye Ulemavu, Getram Kabate juu ya alama mpya kuu za makundi matano ya watu
wenye ulemavu za usalama barabarani.
Kikosi kazi ambacho leo kilikuwa kikitoa elimu ya
Usalama barabarani katika Maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani mjini Iringa..
Kwa lugha fasaha unaweza kumuita Fahari! Huyu dume la
Ngombe ambalo linakadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 1000, akiwa katika
maonesho ndani ya banda la ASAS DAIRY FARM katika uwanja wa Samora mjini Iringa
yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalma kitaifa.
Wakazi
mbalimbali mjini Iringa, wakiangalia Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM
katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalma kitaifa.
Maofisa wa Kampuni ya Airtel Tanzania wakimlisha majani dume la kisasa la Ng’ombe katika banda la ASAS DAIRY FARM
katika uwanja wa Samora mjini Iringa yanapoendelea maonesho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalma kitaifa. Mbegu za Ng'ombe hao zinatoka Ujerumani.
0 comments:
Post a Comment