Leo darasa la saba wanafanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi nchini kote. Takribani robo tatu ya wahitimu haao kila mwaka hufanikiwa kuendelea na elimu ya Sekondari na waliosalia hubaki majumbani na kusaidia wazazi au walezi wao kazi mbalimbali.
Pichani ni Mtoto mkazi wa Mjini Iringa anawakilisha maelfu ya Watoto wa umri wake ambao miaka ya nyuma walihitimu elimu ya msingi na kukosa nafasi ya kuendelea na elimu ya juu na kuamua kujishughulisha na ufanyaji wa biashara ndogo ndogo kama hii ya kuuza mayai na nyinginezo kwa lengo la kujipatia riziki na kuongeza kipato cha familia badala ya kuzurula mitaani na kuomba omba.
Wengi wa watoto ambao humaliza elimu ya Msingi na kukosa nafasi ya kuendelea na masomo ya Sekondari wamekuwa wakikosa vitu vya kufanya na wazazi au walezi kuwaacha bila kuwapa msingi wa ushauri wa kuweza kujitegemea kimaisha ingawaje familia hizo hukosa kipato cha kuweza kutoa mitaji.
Lakini biashara kama hizi zitawaondolea tatizo la kujiingiza katika makundi yasiyo faa.
Kijana akiwa amebeba boksi lililo na bidhaa mbalimbali ambazo huziuza mitaani na wakati mwingine vijana kama huwa huuza bidhaa zao katika magari yafanyayo safari za mikoani.Vijana hawana budi kujitafutia riziki kwa njia halali kama hizi ili kujiepusha na vitendo vya kushinda vijiweni na kuangukia katika uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.
0 comments:
Post a Comment