Uzao wa THT, na huyu ni mwadada
machachari anaekuja kwa kasi Rachel, akipagawisha juu ya jukwaa madhubuti la SERENGETI FIESTA 2012 ndani ya uwanja wa
Samora mjini Iringa hivi sasa.
Bongo movie wakiwa jukwaani
Shilole akiserebuka
Aunt Ezekiel we acha tu
Ray huyoooo akikamua
Wema nae aliimba za Diamond
Diamond akikamua jukwaani
Sheta akimchezesha Diamond
Msanii funga kazi wa Hip Hop, Roma Mkatoliki akikamua
jukwaani kwa staili yake ya kidole cha mwisho juu, Tamasha la Serengeti Fiesta
2012, ndani ya uwanja wa Samora mjini Iringa usiku huu.
Msanii
wa Kizazi kipya Ben Paul akifanya makamuzi yake ndani ya Uwanja wa
Samora mjini Iringa katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Linah akiimba mbele ya mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Iringa
Nimakamuzi ya kiutu uzima kutoka kwa Linah ambaye pia ni zao la THT.
Mkali
Stamina nae akifanya makamuzi jukwaanikatika show kali ya Serengeti
Fiesta Iringa usiku huu wa Septemba 23/24 uwanja wa Samora
DJ PQ akifanya makamuzi yake stegini
Mwanadada
Linah akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Clouds TV, Nickson ambaye
anawika katika Kipindi chake cha Weekend Chart Show!
Hapa wakazi wa Iringa
wakimwangalia Tausi, mwana dada ambaye naweza kusema ni mfupi kuliko wote ambao
nimekwisha wahi kuwaona maishani mwangu.
Mkali Lenex akifanya vitu vyake
jukwaani, hakika Serengeti Fiesta Iringa ni Bhaaaaass!!
Haya sasa MC wa Show Baba Johnniiiie!! akifanya kazi yake na kukubalika na mashabiki hapo chini.
Ni mkali mwingine kutoka jijini Mwanza kupitia shindano la
Serengeti Supa Nyota 2012, Young KIller akikamua vilivyo mbele ya wakazi
wa mji wa Iringa wanaondelea kutinga hivi sasa ndani ya uwanja wa
samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta
2012.
Ni
mkali mwingine kutoka Morogoro kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo
Maker akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa wanaonelea kuingia hivi
sasa ndani ya uwanja wa samora,kutibwirika pamoja na muonekano mpya wa tamasha
la Serengeti Fiesta 2012.
Mmoja wa
wasanii chipukizi aliyeibukia kwenye shindano la Serengeti Supa Nyota
2012,kutoka Mkoani Mbeya aitwaye Ney Lee pichani akionesha kipaji chake
cha kuimba jukwaani usiku huu kwenye uwanja wa Samora,mkoani Iringa
ambako hivi sasa kunarindima tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Wadau wa Serengeti fiesta Iringa na Dar es Salaam nao wapo hapa Uwanja wa Samora Iringa kupata burudani
Ndani ya uwanja wa Samora Mjini Iringa
ndo kwaaaanza kumekucha katika tamasha kubwa na la aina yake ya SERENGETI
FIESTA 2012 ambapo linajiachia usiku huu hadi Bhaaaaaass!!
Wameanza kupanda wasanii
chipukizi wa mjini Iringa na vitongoji vyake.
Watu ndo nao kama hivi nab ado wanamiminika
uwanjani.
Kama hujafika uwanjani hapa fika sasa
0 comments:
Post a Comment