Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi akipokea vifaa vya kupimia ulevi kwa madereva kutoka kwa Steve Gannon mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL) katika hafla ya makabidhiano, iliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani, vifaa hivyo vina thamani ya shilingi milioni 60, katika msaada huo pia kampuni ya bia ya Serengeti imetoa vitabu 20.000 vya leseni kwa ajili ya kusaidia wiki ya nenda kwa usalama barabarani inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya jumatatu mkoani Iringa kitaifa, kushoto ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL),Steve Gannon akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, katikati ni Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, kulia Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani Mbarak Abdulwakil.
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya ndani.
Steve Gannon mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia ya (Serengeti SBL) akionyesha jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi huku Waziri wa mambo ya ndani Mh. Dr. Emmanuel Nchimbi, kulia Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya ndani Mbarak Abdulwakil, kulia ni Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mohamed Mpinga na kutoka kulia ni Nandi Mwiyombela Meneja wa Miradi Endelevu na Uwajibikaji SBL na Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda
0 comments:
Post a Comment