Msanii
nyota kutoka nchini Marekani,ambaye alizaliwa mnamo Januari 28 mwaka
1976 nchini Marekani,akitambulika kwa jina la kisanii kama Rick
Ross,lakini jina halisi akiitwa William Leonard Roberts II,atatua nchini
Tanzania hivi karibuni na kutumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la
Kimataifa la Serengeti Fiesta 2012 litakalofanyika Oktoba 6 ndani ya
viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.
Katika
kuhakikisha mambo yanakwenda sawa bin sawia kwa kila idara kuhusiana na
tamasha hilo, waandaaji ambao ni Prime Time Promotions Ltd
wakishirikiana na Clouds Media Group huku mdhamini wao mkubwa ikiwa ni
kampuni ya bia ya Serengeti,wameandaa shamara shamra mbalimbali za
kuhakikisha tamasha hilo mpaka linafika kileleni,linaamsha na kuacha
gumzo la kipekee kabisa miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji
vyake, ikibidi mpaka Kigoma mwisho wa reli kwa namna moja ama nyingine.
Msanii huyo mwenye umahiri mkubwa wa kufloo awapo jukwaani mpaka sasa anatamba na nyimbo/albamu kadhaa kama vile Hold Me Back 2012 God Forgives, I Don't, Hustlin' 2006 Port of Miami Diced Pineapples 2012 God Forgives, I Don't So Sophisticated 2012 God Forgives, I Don't 911 2012 God Forgives, I Don't Stay Schemin 2012 Rich Forever Aston Martin Music.
Nyinginezo ni 2010 Teflon Don DJ Khaled 2008 Trilla Lemme See 2012 So Sophisticated Amsterdam 2012 God Forgives, I Don't Black Magic 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire The Boss 2008 Trilla You the Boss 2011 You the Boss
Touch'n You 2012 Touch'N You Bag of Money 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire.
0 comments:
Post a Comment