Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2012


 Kaimu Afisa Uhusiano wa  wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Hawa Kikeke(kushoto) na Afisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Andrew Dayson (wa pili kutoka kushoto) wakiwasaidia  Maafisa wa Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali ambayo wamekwishachangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nanenane jana mjini Dodoma.
 Afisa Uhusiano wa Chuo Mipango Dodoma Sarah Mmari (kushoto) akimwelimisha Yulis Otto (kulia) utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho wakati mzee huyo alioptembelea banda la Wizara ya Fedha jana katika maonyesho yanayoendelea mjini Dodoma.
 Mtunzaji Kumbukumbu na Mhasibu Abbas Mnyeto  wa Wizara ya  Fedha wakiwasaidia wazee wastafu upande wa Kilimo juu ya taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wanapostaafu jana mjini Dodoma walipokuwa kwenye banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
 Mwanasheria kutoka  Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Emilia Mkubulo(kulia) akimwelimisha mmoja wa wananchi faida za kununua hisa  jana mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
Afisa Masoko kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) Said Mkomwa(kulia) akiwaelimisha wananchi faida za kuwekeza katika mifuko iliyoanzishwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania jana mjini Dodoma walipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonyesho ya wakulima nanenane.
Posted by MROKI On Friday, August 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo