LICHA ya timu ya Yanga kufaya vizuri katika Mashindano ya Kombe la Kagame 2012 lakini kikosi cha Azam ndio kinaonesha kuwa bora zaidi baada ya kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen kuchagua wachezaji Nane kutoka Azam.
Azam ambao pia ni washindi wa pili wa Ligi kuu ya Soka Tanzania bara na Mabingwa wa Muungano, wamefuatiwa na mabingwa wa kagame Yanga kwa kutoa wachezaji 5 na Simba amabo ni mabingwa wa Tanzania bara wachezaji 5, huku Mtibwa Suger ikitoa mchezaji mmoja.
Wachezaji kutoka Azam ni pamoja na John Bocco, Mwadini Ali , Aggrey Morris , Erasto Nyoni ,Mrisho Ngassa , Ramadhan Chombo Salum Abubakar na Deogratias Munishi
Waliounda kikosi hicho cha taifa Stars wakitokea mabingwa wa soka Tanzania bara ni nahodha wa timu hiyo ya taifa na Simba, Juma Kaseja ,Shomari Kapombe , Haruna Moshi , Mwinyi Kazimoto , Ramadhan Singano.
Wachezaji kutoka Yanga ni Pamoja na Kelvin Yondani,Athuman Idd , Frank Domayo ,Said Bahanuzi, Simon Msuva.
Wachezaji wengine walio itwa kuunda kikosi hicho ni pamoja na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na wachezaji wa kulipwa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Congo- DRC).
Wachezaji wote walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata tayari kwa mchezo wao wa kirafiki utakao pigwa Agosti 15 ugenini.
0 comments:
Post a Comment