Meneja wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjo akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti Oysterbay jijini Dar es salaam wakati alipotangaza washindi wa Droo ya 11 ya Vumbua Dhahabu Chini ya Kizibo inayoendeshwa na kampuni hiyo kila wiki ambapo wametangazwa washindi wa Jenereta na Pikipiki katikati ni Tumainieli Malisa kutoka PWC na kushoto Abubakary Maggid kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha.
Meneja wa bia ya Serengeti Lager Bw. Allan Chonjo akiongea na mmoja wa washindi katika droo hiyo katikati ni Tumainieli Malisa ofisa kutoka PWC.
Ni katika droo ya 11 promosheni ya ‘vumbua hazina chini ya kizibo
‘Serengeti Breweries Limited’
Ni wiki ya 11 sasa tangu kuanza kwa promosheni inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ijulikanayo kama ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na Serengeti Breweries Limited’ ambapo leo asubuhi, ilichezeshwa tena droo ya 11 katika ofisi za kampuni hiyo Serengeti Breweries Limited zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo wawakilishi wa kampuni ya kuendesha michezo ya kubahatisha ya Push Mobile, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.
Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya DIAGEO PLC (UK) yaUingereza na kupitia bidhaa zake, Serengeti Premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendelea na promosheni yake ambapo zoezi la makabidhiano ya zawadi hizo limekua likishamiri na kuingia katika sura mpya baada ya kupata mwitikio mkubwa hali inayofanya watu wengi kuendelea kushiriki na kujishindia zawadi mbalimbali katika promosheni hiyo.
Akiongea katika hafla hiyo, meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo, amesema kwamba“ amawishoni mwa wiki iliyopita zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wetu liliendelea hapa jijini Dar es Salaam ambapo tuliwa kabidhi bw. Richard Mbezi zawadi ya Bajaj na Mbaraka Adam alikabidhiwa pikipiki mpya kabisa” alisema Chonjo na kufafanua kuwa bado zawadi ni nyingi za kushindaniwa hadi promosheni hiyo itakapofika kikomo takribani siku chache zijazo.
Washindi wa leo ni pamoja Inocent Paul 25 kutoka Morogoro ambaye amejishindia pikipiki naMwita Nyamahemba 23 kutoka Nyakato Mwanza mwanafunzi wa chuo Tarime TTC, aliyejinyakulia jenereta mpya.
0 comments:
Post a Comment