Nafasi Ya Matangazo

July 30, 2012

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipeana mkono na Mkurugenzi anaemaliza Muda wake wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Richard Wells baada ya kuzindua rasmi mradi huo wa maji katika Hospitali ya Mawenzi, mkoani Kilimanjaro leo. 
 ***************
Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.

Mradi huo umezinduliwa leo na mke wa waziri mkuu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania Mama Tunu Pinda akiwa ndio mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambapo katika kuuzindua mradi huo uliopata kuhudhuriwa na waandishi wa habari,maafisa kutoka ngazi mbalimbali serikalini mkoani hapo na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro, mama Pinda alielezea kufurahishwa kwake na juhudi zinatofanywa na kampuni ya bia ya Serengeti katika kuisadia jamii ya watanzania bila kupendelea upande wowote.

“Mimi nashukuru sana kwamba leo nimepata fursa ya kusema yale niliyonayo moyoni kwa mda mrefu, kwamba kampuni hii ya bia ya Serengeti kwakweli mnafanya mambo makubwa ambayo hata serikali haikutegemea kama mtafanya, mmekua mstari wa mbele sana katika kuisaidia jamii inyowazunguka kwakujenga miradi mikubwa hasa yale yenye tija na na muhimu katika maisha ya kila siku kwa watanzania” aliseam mama Pinda.

Pia amewataka wakazi na watumiaji wa hospitali ya mawenzi mkoani Kilimanjaro na watanzania kwa ujumla kujenga imani na mahusiano mazuri na makampuni binafsi hasa yanayojali wateja wake na wananchi kwa ujumla kama kampuni ya bia Serengeti.

“Ni mwezi mmoja sasa umepita tangu kampuni hii hii yani Serengeti Breweries ilipozindua mradi mkubwa sana wa maji huko mkoani Iringa na ndio maana nawapongeza sana kwamba mnawajali na kuwasaidia watanzania bila kubagua, najua kuwa mliwahi kujenga mradi mkubwa wa maji Mkuranga jiji Dar es Salaam na kwa sababu hiyo sasa ifike mahali jamii ya watanzania waamini na kutambua kuwa kuwepo kwa kampuni ya bia ya Serengeti hapa nchi kumeleta faida kubwa kwa sereikali na kwa jamii hongereni sana Serengeti breweries kwa juhudi zenu za dhati kabisa za kuinua uchumi ya watanzania” alisema mama Pinda.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, amesema mradi huo uliogharimu zaidi ya milioni 50 za kitanzania ulilenga kutoa suluhisho la muda mrefu katika matatizo sugu yayoikumba jamii hususani tatizo la uhaba wa maji safi kwa maendeleo ya maisha ya mtanzania.

“Sisi kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto zinazowakabili watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama, na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya Serengeti imeona hilo na kuamua kusadia kutatua tatizo hilo katika maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa haraka zaidi” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii ni moja yab sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha shukrani zake kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.

Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya bia ya Afrika Mashariki iliyopo chini ya kampuni za Diageo inayoongoza kwa uzalishaji na usambazaji wa vinywaji vikali na kufikia zaidi ya nchi 180 duniani,Serengeti Breweries ikizalisha Serengeti Premium Lager, Tusker Lager, Tusker Malt Lager, Senator, Pilsner, The Kick, Uhuru Peak Lager.

Posted by MROKI On Monday, July 30, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo