Biashara ya uuzaji wa mafuta ya kupikia yanayozalishwa kutokjana na zao la Alizeti kwa mikoa ya Singida na Dodoma linazidi kushiri siku hadi siku hasa kutokana na ukweli kwa mafuta hayo hayana athari katika mwili wa binadamu.
Ulimaji pia wa zao hilo katika mikoa hiyo na mikoa mingi hapa nchini linazidi kushika kasi siku hadi siku, huku wakulima nao wakiwakwepa wanunuzi wa zao hilo wanao walangua.
Wananchi wengi hivi sasa wakisha lima Alizeti yao huipeleka katika mashine na kukamua na kuuza wenyewe mafuta na kupata faida kamili ya zao hilo. Pichani ni mafuta ya alizeti yakiwa sokoni kutoka kwa wazalishaji tofauti mjini Singida.
Lakini ipo haja ya mamlaka zinazohusika na ukaguzi wa vyakula kupita na kukagua mafuta haya kuwa hayachakachuliwi ili yasilete madhara kwa watumiaji licha ya kuamini kuwa yanatokana na Alizeti.
0 comments:
Post a Comment