Baadhi ya madereva wa Jijini Arusha wamelalamikia kitendo cha Halmashauri ya Jiji la Arusha kuruhusu shughuli za ufanyaji biashara kando kando ya barabara nje ya Soko Kuu la Arusha kwa kuwa mara kwa mara kumekua kukitokea kwa ajali na kusababisha hasa ya mali na maisha ya watu.
Madereva hao wameiambia Father Kidevu Blog, kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakigongwa na wengine kufa huku pia wateja nao wakigongwa na magari au pikipiki.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamepanga bidhaa zao kando ya barabara na kuacha nafasi kidogo isiyoruusu magari kupishana, pia kujaza takataka nyingi katika mtar wa maji taka unaopita kando ya barabara hiyo.
0 comments:
Post a Comment