Nafasi Ya Matangazo

July 05, 2012

Mkuu wa wilaya ya Newala, Christopher Magala (katikati) akizungumza katika mkutano wake na Askari Polisi wa Wilaya ya Newala leo. Kulia ni OCD wa Wilaya ya Newala Lisu Ntandu Jingi na kushoto ni  Kupela kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya newala.
 ********
Mkuu wa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, Christopher Magala, leo amekutana na maofisa wa Jeshi la Polisi na askari wa kawaida wilayanni humo na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusiana na kazi na wajibu wao katika jamii.

DC huyo mpya wa newala amesema ameamua kufanya mkutano huo ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha kwake katika kada mbalimbali za jamii na watendaji wa ngazi mbalimbali za serikali.

Magala pia amesema hivi karibuni amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusiana na utendaji wa Jeshi hilo walio na jukumu la Ulinzi wa raia na mali zao.

Aidha Magala amebainisha kuwa dhumuni la kikao chake na Polisi lilikuwa ni kujitambulisha kwao na kuwakumbusha majukumu yao ya msingi kwa jamii yetu.

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi toka kwa wananchi mara tu baada ya kufika hapa Wilayani, juu ya vitendo na huduma zisizo kidhi haja za wananchi wilayani hapa, hivyo nikalazimika kukutana nao na kuwekana sawa nikiwa ni kiongozi wa ulizni na usalama.” Alisema Magala.

Pamoja na mambo mengine kuu wa wilaya huyo alitumia fursa hiyo kuwakumbusha majukumu yao katika jamii kuwa ni ulinzi wa raia na mali zao, kusimamia amani na utulivu uliopo Wilayani. 

Jana DC huyo alikutana na waendesha boda boda mjini Newala pamoja na wapiga debe katika mabasi ya aibiria Wilayani humo, katika kuzungumza nao na kuweka mambo sawa, ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kujitokeza katika Sensa itakayo fanyika baade mwaka huu nchini kote. 
Posted by MROKI On Thursday, July 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo