Nafasi Ya Matangazo

July 10, 2012

Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala amefungua mafunzo ya mgambo katika Kata ya Mnyambe Wilayani  Newala, mkoani Mtwara leo.

Akihutubia wana mafunzo ya mgambo katika Kata hiyo ya Mnyambe, Mkuu wa Wilaya hiyo amewaasa na kuwafafanulia wana mafunzo kwamba, mafunzo hayo ya mgambo yapo kwa mjibu wa sheria namba 147 ya mwaka 1977 na kwa mjibu wa sheria inayounda jeshi la Wananchi (JWTZ) ya mwaka 1966 na hivyo wapuuze upotoshwaji unaotolewa na baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakieneza uvumi kwamba mgambo haupo kwa mujibu wa sheria.

Aidha Magala amesema kushiriki mafunzo ya Mgambo si lazima bali ni hiari ya mtu mwenye kujitokeza na kujiandikisha ili kuwa wakakamavu na kupata walinzi wazuri wa amani katika jamii.

"Mgambo ni jeshi la akiba linaloundwa na raia wazalendo ambao wako tayari kufanya kazi mbalimbali zinazofanywa na majeshi mengine kama kuokoa maisha na mali za wananchi wakati wa maafa," alisema Magala.

Pia DC Magala amewataka wana mafunzo ya mgambo kuwa mstari wa mbele na kuwa mfano katika kutekeleza sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za nchi kwa kuwa na nidhamu kama wanajeshi wengine mara watakapomaliza mafunzo hayo.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewaambia faida zingine watakazopata mara baada ya kumaliza mafunzo ya mgambo ni pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi kupitia mpango wa ulinzi shilikishi/Polisi jamii katika maeneo mbalimbali mijini na vijijini, kupewa kipaumbele pale majeshi yetu yanapotaka kuajiri, na kupata ajira katika makapuni ya ulinzi:

"Serikali imeyaagiza makampuni yote ya ulinzi kutumia wananchi waliopitia mafunzo ya majeshi mbalimbali na mgambo lakini pia majeshi yote yameelekezwa kuwapa kipaumbele waliopitia mafunzo ya mgambo wakati wa ajira zao,” alisema Magala

Baada ya kufungua mafunzo ya mgambo Mkuu wa Wilaya ya Newala ametembelea shule ya Sekondari ya Mnyambe na kuikagua.

Posted by MROKI On Tuesday, July 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo