Nafasi Ya Matangazo

June 11, 2012

 Ofisa Biashara wa Manispaa ya Arusha, Niarira Magunda(kulia) akimkabidhi Mjasiliamali, Sofia Khalfan, Mashine ya kusaga wakati wa kukabidhi ruzuku kwa wajasiliamali wa Safari Wezeshwa katika Viwanja vya Soweto Mkoani Arusha mwishoni mwa wiki.Kutoka Kulia ni Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiliamali, Veronica Mwamunyange,M       eneja wa Bia ya Safari, Oscar Shelukindo na Meneja mauzo wa Kanda wa TBL, Kitio Wilderson.
*******
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)kupitia Bioa yake ya Safari Lager imekabidhi vitendea kazi mbalimbali kwa wajasiliamali 11 walifuzu kupewa ruzuku za Safari Wezeshwa vyenye thamani ya shilingi milioni 50.

Akizungumza katika sherehe ya makabidhiano ya vifaa hivyo jana jijini Arusha katika viwanja vya Soweto Meneja wa Safari Lager Bw.Oscar Shelukindo alisema kuwa shindano hilo la Wezeshwa na safari Lager nia yake kubwa nikuwapatia ruzuku wajasiriamali wadogo na wakati kuendeleza biashara zao.

.Shelukindo alisema jumla ya shilingi milioni 50 zimetumika katika kununulia vifaa hivyo kwa ukanda wa kaskazini, ambapo mwaka 2011 ruzuku ilikuwa ni milioni 200 kama vifaa vya vitendea kazi kwa wajasiriamali hao walioshinda katika shindano hilo.

Alisema kuwa zoezi hilo lilianzia mbeya na Arusha na wanatarajia wiki ijayo kuwa Mwanza na mwisho kumalizia zoezi hilo Dar es Salaam.

Naye Mgeni rasmi katika sherehe hizo,Niarire Magunda ambaye ni Afisa Biashara Manispaa ya Arusha aliipongeza TBL kupitia Bia yake ya Safari Lager kwa kuanzisha programu hiyo yenye nia ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wakati.

“Hakuna mtu aliye maskini, kubwa nikuwezeshwa namna ya kupata fedha hivyo ni vyema kama mtu akapata wazo la ujasiriamali ni bora akafanyia kazi wazo lake ”alisema Magunda.

Hata hivyo katika zoezi hilo wajasiriamali 11 kutoka Arusha,Moshi na Tanga walikabidhiwa vifaa mbalimbali vya vitendea kazi, ambapo wajasiriamali hao ni Bi.Ansilla Danny,Bi.Msuma,Bw.Roger Msangi,Bw.Simon Kinabo,Bi.Sophia Khalfani,Bw.Yuda Mbando,Bi.Amina Lyimo,Bw.Adam Akilinyingi,Bw.Joseph Mnemwa,Bi Rose Tesha na Bi.Victoria Tesha
Posted by MROKI On Monday, June 11, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo