Kampuni inayoongoza kwa mawasiliano, Vodacom Tanzania, inaendelea kuonyesha uongozi wake katika huduma yake ya kutuma na kupokea pesa ya M-pesa, ambayo ni huduma yenye mtandao mpana zaidi wa mawakala, unaoaminika katika kutuma pesa, kupokea pesa na kulipia huduma mbalimbali pamoja na kuhifadhi pesa.
M-pesa ina takribani mawakala 20,000 ambao wamesambaa nchi nzima, M-pesa ni rahisi kutumia na ina wateja wengi zaidi wanaoweza kutumia huduma hii hata wakiwa vijijini.
Vilevile, kampuni imezindua promosheni mbalimbali kwa ajili ya wateja wake nchi nzima, ili kuweza kuwasukuru kwa kuwa wateja wa Vodacom na pia kutumia huduma hii inayorahisisha maisha.
Promosheni hizi zinawapa wateja ofa mbalimbali zikiwemo muda wa nyongeza wa maongezi bure, kuchezesha michezo ya bahati nasibu ambayo husimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
"Tumezindua promosheni mbalimbali ambazo zinawawezesha wateja kuweza kujipatia muda wa maongezi wa ziada bure wanapotuma au kupokea pesa kwa kupitia M-pesa.
"Tumezindua promosheni mbalimbali ambazo zinawawezesha wateja kuweza kujipatia muda wa maongezi wa ziada bure wanapotuma au kupokea pesa kwa kupitia M-pesa.
Hii ni moja ya njia ya kusema 'asante' kwa wateja wetu kwa kutumia na kuamini huduma zetu'' Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza Huduma ya Vodacom M-pesa ilizinduliwa mwaka 2008 na imetoa mchango mkubwa sana kwenye maisha ya Watanzania na kwamba Vodacom M-pesa ni huduma inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu na matumizi yake kuongezeka siku hadi siku na kufanya Vodacom Tanzania iwe chaguo zaidi la ufumbuzi wa masuala ya fedha hapa nchini na nchi zingine.
Bw. Meza ana uhakika kwamba uwekezaji uliokua katika mchakato mwaka huu wa zaidi ya Sh. 130 bilioni ili kuboresha mtandao utasaidia kuweza kufanya bidhaa na huduma za Vodacom kupatikana zaidi maeneo yote ya nchi, Watanzania wengi zaidi wataweza kutumia huduma hii nzuri.
Ni wikiendi hii tu iliyopita, Kampuni ilifanya maboresho kwenye mtandao wa M-pesa nchi nzima ili kuhakikisha kuwa wateja wanaendelea kunufaika na kufurahia huduma hii.
0 comments:
Post a Comment