Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sofia Productions,Mussa Kisoky akisisitiza jambo wakati akitoa taarifa ya maandalizi ya Tamasha hilo la Grand Malt Film Festval Tanzania linalotarajiwa kufanyika jijini Tanga jumamosi hii.Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah na kulia ni Mmoja wa Wacheza Filamu hizo watakaoonyesha kazi zao katika Tamasha hilo,Vicent Kigosi a.k.a Ray.
JB akizungumzia Tamasha hilo.
********
Kinywaji cha Grand Malt leo kimetangaza kuendelea kudhamini tamasha maarufu la Filamu hapa Tanzania lijulikanalo kama “Tanzania Open Film Festival” (TOFF) ambalo hufanyika jijini Tanga kila mwaka.
Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha la mwaka huu, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam alisema; Kinywaji cha Grand Malt ndiye mdhamini mkuu wa Tamasha la Filamu Tanzania.
Tamasha hili limekuwa likifanyika katika Jiji la Tanga na limeonesha kupendwa sana na wakazi wa Jiji la Tanga. Kwa mwaka huu wa 2012, tamasha hili linaanza tarehe 30 June hadi tarehe 6 Julai.
Kwa kipindi chote hiki, Grand Malt imejipanga kuhakikisha kuwa tunafanya uhamasishaji wa kutosha katika jiji la Tanga, ili kuwawezesha wakazi wa Tanga na maeneo ya jirani kuweza kuhudhuria tamasha hili.
Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za kitanzania kufika na kushuhudia Tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi.
Nae Meneja Masoko wa TBL, Bw. Fimbo Butallah alisema; Kama mtakumbuka, Mwaka jana Grand Malt iliamua kushirikiana na Kampuni ya Sophia Records, ambao ndio waandaaji na waasisi wa Tamasha hili.
Ushirikiano wetu ulikuwa mzuri, kwani tulijifunza mambo mengi juu ya Tamasha hili, lakini kikubwa zaidi tulijionea jinsi wananchi wanavyozipenda sana filamu za Kitanzania almaarufu kama “Bongo Movies” na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa Bongo Movies ana kwa ana.
Kufuatia umuhimu huo hatua ya kwanza tuliyochukua ni kusaini mkataba wa udhamini wa miaka mitatu na kampuni ya Sophia Records, na hatua nyingine itakuwa kuweka utaratibu wa kulipeleka Tamasha hili katika mikoa mingine ya Tanzania na hatimaye kuliweka katika hadhi ya kimataifa.
Grand Malt inawaahidi wakazi wa Tanga na Watanzania wote kwa ujumla, kuwa Tamasha hili litakuwa na mvuto wa aina yake na hatimae kutumika kulitangaza Taifa letu kupitia tasnia hii ya filamu ambayo kwa sasa inakua kwa kasi kubwa.
Nae Mkurugenzi wa Sophia Records, waandaaji na waasisi wa Tamasha hili, Bw. Musa Kissoky alisema; kwanza kabisa tunatoa shukurani za dhati kwa Grand Malt kwa kukubali kushirikiana nasi katika kuboresha na kuendeleza Tamasha hili.
Sophia Records iliona kiu ya watanzania kupata fursa ya kuona filamu za wasanii wetu hasa katika jukwaa kubwa la wazi, lakini pia kukutana na wasanii wenyewe na kubadilisha na nao mawazo juu ya tasnia hii, hivyo tukaanzisha Tamasha hili ambalo sasa linajulikana kama “Grand Malt Tanzania Open Film Festival”.
Tunawashukuru saana wasanii wa Bongo Movies, hususan uongozi wao, kwa ushirikiana mkubwa wanaotupatia katika kuhakikisha mafanikio ya matamasha haya.
Akizungumzia maandalizi ya Tamasha la mwaka huu linaloanza Juni 30, alisema; maandalizi yote yapo tayari, kama ilivyo kawaida, Tamasha litafanyika katika viwanja vya Tangamano na litakuwa likianza asubuhi hadi usiku.
Tumeandaa burudani nyingi zitakazosindikiza maonesho haya ya Filamu kwa siku zote saba, na hakutakuwa na kiingilio, hivyo watu wote wanakaribishwa kuja kujionea Filamu zetu na kukutana na wasanii waliobobea katika tasnia hii ili wabadilishane mawazo.
0 comments:
Post a Comment