Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah (katikati)
akiongea na Waandishi wa habari wakati wa uzunduzi wa Tuzo za Excel with
Grand Malt kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini leo kwenye ukumbi wa
Mikutano wa TBL,jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Kinywaji
hicho,Consolata Adam na kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa
TBL,Edith Mushi.
Kiwanji cha Grand Malt kisicho na kilevi leo kimezindua tuzo za 'Exel with Grand Malt" kwa wanafunzi wa elimu ya juu ikiwa ni mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambapo jumla ya sh. milioni tano zimetengwa kuwazawadia watakaoshinda. Pichani, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) inayotengeneza kinywaji hicho, Fimbo Butala akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, jana kuhusu promosheni hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi.
Kinywaji
maarufu cha Grand Malt leo kimezindua tuzo kwa wanafunzi wa elimu ya
juu zijulikanazo kama “Excel with Grand Malt”, huu ukiwa ni mwaka wa
pili kwa tuzo hizi kutolewa.
Akizungumzia
tuzo hizo, meneja wa kinywaji cha Grand Malt Bi. Consolata Adam
alisema; Excel with Grand Malt ni tuzo za aina yake ambazo zimelenga
kutambua na kuthamini mchango wanaoonesha wanafunzi katika fani
mbalimbali nje ya masomo ya darasani.
Tunatambua
kuwa kazi kubwa ya mwanafunzi anapokuwa chuoni ni kuhudhuria vipindi
vya darasani na kupata elimu, bali tunapenda pia kuwatambua wale
wachache ambao wanakwenda mbali zaidi na kufanya mambo ya maendeleo
katika mazingira yao ya chuo.
Tuzo
hizi zilianzishwa mwaka jana ambapo tuliweza kufika katika mikoa sita
na kufikia vyuo vipatavyo ishirini. Kwa mwaka huu mchakato utaanza mwezi
Aprili hadi June, na Mikoa itakayohusika ni pamoja na Dar es salaam,
Morogoro, Iringa, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo vyuo vipatavyo 21
vitashiriki.
Kama
ilivyokuwa mwaka jana, fani zitakazoshindanishwa ni Ubunifu
(Innovation), Michezo (sports), Utamaduni na burudani (Culture &
Entertainment) na Mazingira na Huduma za jamii (Environment & social
responsibilities). Kama ilivyo ada, washindi katika fani hizi
watajipatia zawadi mbalimbali toka Grand Malt ikiwa ni pamoja na pesa za
kununulia vitabu na vyeti vya ushindi.
Kwa
sasa natangaza rasmi kuwa tunzo hizi zimezinduliwa rasmi na mkoa wa
kwanza utakuwa ni Morogoro ambapo tunatarajia kufanya tamasha kubwa
kwenye viwanja vya chuo kikuu cha SUA siku ya jumamosi kisha jumapili
tutafanya tamasha la ufunguzi kwenye Viwanja vya chuo cha CBE mkoani
Dodoma na kutakuwa na burudani zitakazoongozwa na nguli wa Hip hop
nchini Joh Makini ,zawadi nyingi na zaidi kutakuwa na GrandMalt baridi
na hakutakuwa na kiingilio chochote. Alisema Bi. Consolata.
Akielezea
umuhimu wa Tuzo hizo, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema;
Tunafurahi sana kuona vyuo vyote vilipokea tuzo hizi kwa furaha kubwa,
hii ni kwa sababu wanatambua umuhimu wake. Kupitia tuzo hizi ambazo
zitakuwa zikitolewa kila mwaka, Grand Malt inatoa changamoto kwa vijana
walio vyuoni kuona umuhimu wa kujituma na kufanya mambo mengi na makubwa
zaidi ya kufaulu mitihani ya darasani tu.
Tunaomba
viongozi wa serikali za wanafunzi na viongozi wa vyuo kuendelea kutoa
ushirikiano kama walivyofanya mwaka jana ili kuleta ufanisi zaidi katika
tuzo za mwaka huu. Kama ilivyo kawaida, utaratibu utakuwa ule ule
ambapo wanchuo watapendekeza majina ya vijana wanaoamini kuwa wamefanya
mambo makubwa ndani ya vyuo vyao katika tasnia zilizotajwa hapo awali,
kisha kufuatiwa na kipindi cha kupiga kura ambapo washindi watapatikana.
Alimaliza Bw. Butallah
Kwa
upande wake meneja mahusiano na mawasiliano wa Tbl Bi Edith
Mushi,Alisema GrandMalt kwa kuzingatia umuhimu wa juhudi za serikali
katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti mwaka huu
Grand Malt itafanya zoezi maalum kwenye kila chuo kwa kupanda miti imara
itakayosaidia kutunza na kuboresha mazingira ya vyuo hivyo ili kuandaa
mazingira bora ya kusomea ya wanafunzi wa sasa na wa vizazi vijavyo
ambapo mkoani Dodoma zoezi hilo litafanyika jumatatu May 07,2012 katika
vyuo vya UDOM na CBE tawi la Dodoma na Mkoani Morogoro zoezi hilo
litafanyika kwenye vyuo vya SUA na Mzumbe siku ya jumanne May 08,2012
asubuhi, kisho zoezi hilo litaendelea katika mikoa ya
Iringa,kilimanjaro,Mwanza na Dar Es Salaam.
0 comments:
Post a Comment