John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.
BAVICHA
imepokea kwa mshituko mkubwa kauli ya ndugu Shibuda kuwa yeye atagombea
Urais na Meneja wake wa Kampeni atakuwa Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya
Kikwete, na alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM.
MAMBO YAFUATAYO YEMETUSHTUA;
1. Katoa Kauli hiyo kwenye kikao cha NEC ya CCM
2. Meneja wa kampeni zake amemtangaza kuwa ni Mwenyekiti wa CCM taifa Jakaya Kikwete
3. Amesema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuiongoza nchi kwa sasa
4. Alitoa tamko hilo kwa niaba ya APRM .
Mambo
hayo manne ndio yametushtua na kutufedhehesha sana sisi vijana wa
CHADEMA na ndio maana tumelazimika kutoa kauli kuhusiana na suala hili ,
na kauli yetu ni kama ifuatavyo;
1. Kamwe
BAVICHA hatutaruhusu mgombea Urais wa CHADEMA meneja wake wa kampeni
awe ni Mwenyekiti wa CCM hata siku moja kwani tunao watu wa kutosha na
wenye uwezo wa kutosha kuifanya kazi hiyo na hatuhitaji msaada huo .
2. Kamwe
hatutaruhusu mgombea urais wa CHADEMA awe anatangaza nia kwenye vikiao
vya CCM kwani hawana mamlaka ya kumteua mgombea wa CHADEMA na kama
Shibuda alikuwa halijui hilo anapaswa kulifahamu kuanzia sasa kuwa
vijana wa CHADEMA hatuchaguliwi mgombea na NEC ya CCM kwani CHADEMA kuna
vikao na taratibu zetu za kuteua wagombea.
3. Kusema
kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuongoza nchi ni
kutudhalilisha sisi vijana wa CHADEMA na watanzania wote ambao leo
wanaiona CHADEMA kama tumaini pekee la kuwakomboa, kauli hii tunaamini
kama vijana wa CHADEMA kuwa mamlaka za nidhamu hazitakaa kimya na
kuiachia kauli ya namna hii iachwe bila kutakiwa maelezo ya kina ,
tutaitisha kikao cha BARAZA na tutaijadili kauli hii na kuwasilisha
mapendekezo yetu kwenye vikao halali vya chama .
4. Tunapenda
kumwambia kuwa kama anaona kuwa yeye haendani na utamaduni wa chama
chetu na anakiona kuwa hakina uwezo wa kuongoza dola anafanya nini
kwenye chama ambacho anona kuwa hakiwezi kuongoza dola? Kwanini atafute
urais kwenye chama ambacho anaona hakiwezi kuongoza dola ? anawatania
watanzania? Ni heri akaenda kwenye hicho ambacho anaamini kuwa kinaweza
kuongoza dola , kwani lengo la chama chochote kile ni kuchukua dola na
sio vinginevyo.
5. Mwisho
tunapenda kuwahakikishia vijana wote wa Tanzania na wananchi kwa ujumla
kuwa tayari CHADEMA kimejiandaa kikamilifu kuongoza dola na wasiwe na
hofu na maneno yaliyotamkwa na Mbunge huyu .
6. Natoa
wito kwa Vijana wenzangu wote wa CHADEMA kuwa sasa tujiandae kikamilifu
katika kukabiliana na mtu yeyote yule ambaye ataonekana kuwa kikwazo
kwa chama chetu na wananchi kwa ujumla wake katika kuelekea kuchukua
dola 2015 .
Nawatakia kila la kheri katika ujenzi wa chama na tuendeleze operesheni ya ‘Vua Gamba, Vaa Gwanda’ popote pale tulipo nchini.
Imetolewa leo Dar es Salaam, Mei 16, 2012 na;
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.
0 comments:
Post a Comment