Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana wa Chama hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
Wanachama wa Chadema pamoja na washabiki wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo wakishangilia ushindi wa kesi ya Mbunge wao,Mh. John Mnyika.
Askari Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia walizokuwa wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge wao.
Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Mahakama Kuu Kanda ya dar es Salaam leo imemtangaza mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema) kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo.
Hayo yamesemwa masaa machashe yaliyopita na Katika Mahakama Kuu na Jaji Upendo Msuya katika hukumu ya kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnyika iliyokuwa imefunguliwa na Hawa Ng'humbi ambaye alikuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo hilo.
Jaji huyo amesema kuwa mdai ambaye ni Nghumbi alishindwa kuthibitishia Mahakama kuhusu kesi dhidi ya Mnyika katika madai yake matano aliyokuwa aliyawasilisha mahakamani hapo na hivyo mahakama hiyo imeamuru gharama za kesi hiyo zitalipwa na Ngh'umbi.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo Ng'humbi alisema kuwa hawezi kusema kama ameridhika au laa kwa wakati huo.
Kwa upande wa chadema ilikuwa ni Sherehe ya ushindi,huku Mnyika akiondolewa kwa kubebwa na wana Chadema waliokuwa wamejaa mahakamani hapo ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho,Freeman Mbowe alisema kuwa ameridhika na hukumu hiyo na kukiri kuwa mahakama imetenda haki.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

0 comments:
Post a Comment