Nafasi Ya Matangazo

May 03, 2012

Shindano la kumsaka mrembo waTabata, Miss Tabata 2012, litafanyika Juni 1 katika ukumbi wa Da West Park,Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho hilo pia kutakuwa na sherehe kabambe yakusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.

“Shindano la mwaka huu litakuwani la aina yake kwa sasabu hii itakuwa ni mwaka wetu wa 10 kuanda Miss Tabata.Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi. Pia tutahakikishatunashirikisha warembo bomba wenye hadhi ya kushinda taji la Miss World,”Kapinga alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.

Kapinga alisema kuwa warembowaliyowahi kushinda mataji tofauti tofauti la shindano hilo pia watakuepo kusherekea miaka 10 yaMiss Tabata.

Warembo watakaoshiriki kwenyeshindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.

Warembo hao ni Neema Saleh (18), Noella Michael (19), Queen Issa(20), Hycalisa Joseph (18), Phillios Lemi (19), Wikllihemina Mvungi (20) naNightness Rajab (19). Wengine ni Suzanne Pancras (19), Caroline David (21),Khadija Nurdin (19), Jamila Omary (18), Advent Mamkwe (21), Nadya Marjeby (21), Axer Peter (20), Rahama Hassan (19),Mercy Mlay (21) na Diana Simon Laizer (20).

Kapinga aliwaomba warembo wenyesifa kuendelea kujitokeza waweze kupata wawakilishi bora katika shindano laKanda ya Ilala.

"Bado milango iko wazi,mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindanola mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza.

Warembo 10 watachaguliwakushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.

Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni  Faiza Ally.

Warembo wa Tabata wamekuwawakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juziConsolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wakinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishindanafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.

Juliet ndiye anayeshikiliataji la dunia la Miss Progressive International.
Posted by MROKI On Thursday, May 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo