Tanzania leo imeungana na nchi nyingine
ulimwenguni kufanya maadhimisho ya siku ya Familia, hapa nchini watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi bila ya uangalizi wa Wazazi au walezi imekuwa
ikiongezeka siku hadi siku.
Leo hii Camera ya FK Blog ilimulika watoto
hawa wa Mjini Singida ambao maisha yao ni sawa na ndege, hawajui wanakula nini,
wanavaa nini, kuoga au mahali pa kujilaza.
Wengi wanawaita watoto wa Mtaani, lakini
ukweli ni kuwa hakuna mtoto wa mtaani, bali watoto wote wanatoka katika familia
ambayo ni muungano wa Baba na Mama. Panapotokea mifarakano ya waanzilishi wa
familia na kila mmoja kwenda ajuako, ndipo watoto nao huingia katika maisha ya
malezi ya upande mmoja.
Mahojiano ya kila matra yanayofanywa na
vyombo vya habari na wataalam wa mambo ya Ustawi wa jamii hubaini kuwa wingi wa
watoto hao mtyaani ni chimbuko la mifarakano ya wana familia wawili.
Baba anapo mtaliki mama na kuoa mke mwingine
amekuwa akileta unyanyasaji na kufanya motto kukimbia nyumbani, kadhalika pia
mama akiolewa sehemu nyingine baba wa kurithi hana mapenzi na malezi bora kwa mtoto.
Jamii haina budi kubadilika na kutatua
migogoro ya familia na kuzaa kabla ya wakati na kushindwa kutoa huduma bora kwa
watoto wa namna hii.
Hawa ni watoto wetu na si watoto wa mtaani,
tuwalee!
0 comments:
Post a Comment