Nafasi Ya Matangazo

May 03, 2012

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imethibitisha kuwa Mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga (CCM), ni Mbunge halali wa jimbo hilo na uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, 2010 na kumpa ushindi, ulikuwa wa halali.

Jaji Profesa Ibrahim Juma aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Chadema, Fred Mpendazoe, alitoa uamuzi huo jana baada ya kumaliza kusikiliza ushahidi wa pande hizo mbili.


“Maombi ya mdai yamekataliwa na yanatupwa … natamka kuwa Mahanga alichaguliwa kihalali na cheti kikatolewa,” alisema Jaji Juma ambaye pia ameamuru gharama za kesi hiyo zibebwe na Mpendazoe.


Ulinzi mkali Nje na ndani ya jengo la Mahakama Kuu ya Biashara ambako kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa, baada ya jengo la Mahakama Kuu kuwa katika ukarabati, kulitanda askari huku watu wengi wakijazana kusikiliza hukumu hiyo.


Hata hivyo, baada ya hukumu hakukuwa na vurugu yoyote isipokuwa wafuasi wa CCM waliondoka wakiimba na kushangilia ushindi wa Mbunge wao.


Katika hukumu hiyo aliyoisoma kwa zaidi ya saa mbili, Jaji Juma alisema anatupilia mbali hoja zote 11 zilizowasilishwa na Mpendazoe, kwa sababu hakuna hata moja aliyoithibitisha na kwamba anatamka uchaguzi ulikuwa wa haki na ulifuata taratibu zote. Masanduku ya kura Kuhusu madai kwamba Dk. Mahanga alikamatwa na masanduku ya kura, Jaji Juma alisema hoja hiyo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.


Alifafanua kuwa hoja hiyo haina ushahidi wowote kwa kuwa mashahidi wengine walidai alikamatwa Kimanga na wengine Buguruni.


“Kwa tuhuma hizo ina maana msimamizi hakuwa makini, jambo lililosababisha masanduku kuibwa suala linalofanya uvumi usitiliwe maanani. Kama kweli jambo hilo lilikuwa wazi kiasi hicho, kwa nini hakujitokeza mtu kutoa ushahidi kuthibitisha Mahanga kukamatwa?” Alihoji.


Alisema shahidi wa Mpendazoe, Aziza Masoud ambaye ni mwandishi wa habari, alidai alipata fununu hizo akaenda kituo cha Polisi Buguruni kujiridhisha. 
Soma zaidi HABARILEO. 
Posted by MROKI On Thursday, May 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo