Nafasi Ya Matangazo

March 26, 2012

 Salim Asas Abri akiwa katika moja ya mazizi ya Ng'ombe wake Kijiji cha Nduli mkoani Iringa.

Unapozunguzia wafugaji nchini wa kisasa na wazalishaji wakubwa wa bidhaa zitokanazo na Ng’ombe hapa nchini katu huwezi liacha jina la kampuni ya Asas ya mjini Iringa.

Asas ni moja ya makampuni makubwa hapa nchini yanayomilikiwa na mtu binafsi na yanayofanya kazi ya ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa na nyama.

Asas wazalishaji wakubwa wa maziwa fresh, Mtindi ulio katika ladha mbalimbali, Jibini, Samli na Siagi hapa nchini ambayo huzalisha mkoani Iringa lakini hivi sasa sifa zake zimeanza kupasua anga la kimataifa.

Hivi karibuni Blogu hii ya Father Kidevu, ilipata fursa ya kutembelea mashamba mawili kati ya matatu ya Mfugaji na mfanbya biashara maarufu wa mjini Iringa ASAS na kujionea ufugaji wa Ngombe wa kisasa ambao huleta mazao bora na yauhakika.

Ni katika eneo la Nduli nje kidogo ya mji wa Iringa lakini ni ndani ya Manispaa ya Iringa ndipo unaanza kukutana na shamba kubwa la mifugo la Asas, mkono wako wa kulia kama unaelekea Uwanja wa Ndege. Lakini mbele kidogo ukipita uwabja wa ndege wa Nduli pia unakutana na shamba linguine kubwa lililo ndani kidogo.
Ndama waliozalishwa katika Mashamba ya mifugo ya ASAS mkoani Iringa wakikuzwa kwaajili ya nyama.
Ni shamba hili mablo FK Blog ilifanikiwa kuingia na kujionea mang’mbe ya hatari. Ndio wa hatari maana Ndama tu wa mwaka 1 analingana na Ng’ombe wangu niliozoea kuwaona mtaani na Yule wa miaka miwili ni mkubwa sana na nilipouliza uzito wake niliambiwa ana takriban tani moja. (Kg.1,000).

Huyu ni ng’ombe dume aina ya Simmental, ambao asili yake ni Amerika ya Kaskazini ambako walikuwa wakizalishwa tangu mwanzani mwa karne ya 20.

Tulipata fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya ASAS, Bw. Salim ‘Asas’ Abri na kusema kuwa Ng’ombe hao huwafuga kwaajili ya kuwauza kwa wafugaji walio na uhitaji wa kupata mbegu bora ya mifugo. Na yeye huagiza mbegu za Ng’ombe hao kutoka nchi za Ulaya hasa Ufarasa na Amerika.

Pia anadai hivi sasa anazalisha zaidi Ng’ombe wa maziwa nyama, ili kukidhi mahitaji yake ya maziwa kwa siku ambayo huhitajika kiwandani.

“Hivi sasa maziwa ninayo zalisha katika mashamba yangu hayakidhi kabisa mahitaji ya kiwandani, hivyo nanunua pia kutoka kwa wafugaji wenzangu wadogo na wakubwa. Lakini bado mahitaji ni makubwa na hayatosho,” anasema Abri.

Aidha Abri anasema kuwa wanazalisha na Ng’ombe wa Nyama na mambo yakienda vizuri wanaweza kufungua kiwanda cha kuzindika nyama.
  
Mkurugenzi huyo wa ASAS anasema kuwa hivi sasa bidhaa zao zimeanza kuingia katika soko la kimataifa kwani Kampuni za ndege zimeanza kuchukua bidhaa zao na abiria wameonesha kuzipenda zaidi.


Ng’ombe wa kisasa wa maziwa anepatikana katika shamba la Asas

Farasi waliopo katika shamba la ASAS la Igingilani mkoani Iringa.

Nyati wakiwa katika banda lao katika shmba la Igingilani
Maziwa ya Ngamia yanaaminika kuwa ni maziwa mazuri sana kwa tiba, nao wanapatikana.
Posted by MROKI On Monday, March 26, 2012 1 comment

1 comment:

  1. FK, HII HABARI NIMEITAFUTA SANA. NILIMUONA HUYU BWANA KWA KIFUPI SANA NILIPOFUNGUA TV YANGU NA KUKUTA HABARI YENYEWE IKIISHIA. NATAKA SANA KUFUGA NG'OMBE, JE NITAWAPATA HAPO KWA ASAS? NA ASAS WENYEWE NITAWAPATAJE, MAANA NIMETUMA EMAIL KWA ADDRESS ZAO LAKINI SIJAPATA JIBU MPAKA LEO. TAFADHALI NIJULISHE.

    BEN

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo