Nafasi Ya Matangazo

February 10, 2012

WARSHA YA UANDISHI WA MISWAADA YA FILAMU/SCREENPLAY WORKSHOP(Level 1)

Je ?unajua kuwa hadithi za Filamu zozote hujengwa kwa wahusika, wahusika ndiyo wabeba lengo zima la filamu? je wajua jinsi ya kuwajenga wahusika wako ili waweze kubeba lengo la hadithi ya Filamu kiufasaha? 

je unajua kuwa ukikosea kumjenga mhusika mkuu katika hadithi ya Filamu yako ni vigumu hadithi ya Filamu bora? basi ukitaka kuyajua yote haya karibu katika warsha ya uandishi wa miswada  ya filamu pale IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Kuanziatarehe 13-15 Februari2012 ,Kutakuwa naWarsha ya Uandishi wa Miswaada ya Filamu/Screenplay Workshop(Level 1) , Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kila siku kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana , Cheti cha Ushiriki kitatolewa mwishoni mwa mafunzo.

Warsha itakuwa kwa Kiswahili (na Kiingereza ikibidi) na mshiriki anaweza kuwa mtu yoyote anayependa kuandika miswada ya filamu (amateur scriptwriter) au mwandishi anayechipukia (upcoming scriptwriter).

Hima wadau wote wa Tasnia ya Filamu ,Sanaa, Sanaa za Maonyesho na Uandishi wa ubunifu msikose nafasi hii muhimu ya warsha mafunzo daraja la kwanza ili kujijengea misingi mizuri ya Uandishi wa Miswaada yaFilamu

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na warsha hii tafadhali wasiliana na IDARA YA SANAA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM ,Ndg.JohnMwakilama, SimuNamba0714 13 22 49, na baruapepe :mwakilamajohn@yahoo.com
Posted by MROKI On Friday, February 10, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo