Meneja Masoko wa Coca-Cola Tanzania Salome Mabirizi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Coca-Cola ‘teen parties’ au Waka Waka na Coca-Cola inayojumuisha vijana wenye umri kati ya miaka 13 na 19. Lengo ni kuwapa fursa vijana kuonyesha ubunifu wao katika mambo mbali mbali kama vile burudani. Uzinduzi rasmi wa teen parties unafanyika Mwanza kesho Jumamosi Februari 11 ambapo mwanamuziki nyota wa kizazi kipya Mwasiti Almasi atatumbuiza. Kushoto ni Aba Seduu wa Scanard ambayo ndiyo kampuni inayoratibu teen parties.
Aba Seduu wa kampuni ya Scanard Tanzania akielezea jinsi ambavyo Coca-Cola teen parties zitakavyoendeshwa nchi nzima kuanzia kesho Jumamosi Februari 11 ambapo burudani hizo za vijana zitazinduliwa rasmi jijini Mwanza na kutumbuizwa na mwanamuziki nyota wa kizazi kipya Mwasiti Almasi. Lengo ni kuwapa vijana fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika mambo mbali mbali kama vile burudani. Kulia ni Meneja Masoko wa Coca-Cola Tanzania Salome Mabirizi.
0 comments:
Post a Comment