Mlima Kilimanjaro kama unavyoonekana katika picha zilizopigwa kwa siku mbili tofauti. Mpigaji wa picha hizi Mroki Mroki ama Father Kidevu, alizipiga picha hizi Februri 20 picha ya Chini na 21 picha ya juu akiwa katika miinuko ya Ugweno Msangeni Wilayani Mwanga mkaoni Kilimanjaro.
Mbadiliko ya tabia nchi ambayoyanapelekea joto kuongezeka nchini yanasababisha kuyeyuka kwa seruji ambayo daima huwepo juu ya kilele cha mlima huo na kushuka chini na kuufanya manzari ya mlima huo kuwa ya kuvutia.
Kuyeyuka kwa seluji hiyo kunafanya baadhi ya maeneo ya mji wa Moshi kuwa na joto kali tofauti na miaka ya nyuma ambako Moshi huwa na baridi kali.
Lakini kutokana na picha hizi hali ya hewa leo hii Februari 21, 2012 inaonesha kuwa nzuri kiasi cha seruji kurejea katika mlima huo kutwa nzima ya leo.
Eneo la milima ya Ugweno kama linavyoonekana katika picha hizi mbili.
0 comments:
Post a Comment