

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani (SACP),Mohamed Mpinga akizungumza mapema leo jijini Dar,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya usalama barabarani (pichani chini),iliyoandaliwa na Rotary Club wakishirikiana na Jeshi la Polisi,kitengo cha Usalama Barabarani sambamba na makampuni mbalimbali ikiwemo na kampuni ya simu za mikononi ya Airtel.Kamanda Mpinga alisema kuwa anawashukuru sana wadau wote waliojitokeza kuunga mkono kampeni hiyo ambayo ni mahususi kabisa katika suala la zima la kuhakikisha ajali zinapungua barabarani kadiri iwezekanavyo.

Mkurugenzi Miradi wa Rotary Club,Bw.Zainul Doss akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali waliofika na kuifanikisha hafla ya uzinduzi huo leo jijini Dar.


Meza kuu kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo.

Baadhi ya wageni waalikwa kutoka Rotary Club.

Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo wa kampeni mpya ya usalama barabarani iliyoandaliwa na Rotary Club kwa kushirikiana na jeshi la polisi,kitengo cha Usalama barabarani wakifuatilia tukia hilo kwa makini.




0 comments:
Post a Comment