Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2012

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki amewaomba raia wake kuwa watulivu baada ya Mahakama ya kimataifa ya jinai, ICC,  ilioko The Hague kutoa uamuzi juu ya watuhumiwa sita wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini humo. 

Mahakama hiyo imesema watuhumiwa 4 kati ya 6 waliokuwa wanakabiliwa na shutma hizo wana kesi ya kujibu juu ya kutokea kwa ghasia nchini kenya mwaka wa 2007 na 2008.

Rais Kibaki amesema wakenya wabakie watulivu na wenye amani na kwamba tayari Kenya imepitia changamoto nyingi na kwamba taifa hilo halipaswi kurejeshwa nyuma kwa machafuko.

Wanne hao watakaokuwa na kesi ya kujibu juu ya ghasia za baada ya uchaguzi ni naibu waziri mkuu, Uhuru Kenyatta; aliyekuwa waziri, William Ruto; mwandishi wa habari, Joshua Arap Sang; na mkuu wa utumishi wa serikali, Francis Muthaura.
Source... http://www.dw-world.de
Posted by MROKI On Monday, January 23, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo