Nafasi Ya Matangazo

January 23, 2012

Mjalojia mkuu wa kampuni ya Mantra Tanzania,Emauel Nyamsika (aliyeinama) akiwaonesha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Ruvuma,wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo,Mh. Said Mwambungu (wa nne kulia) ramani maalumu inayoonesha maeneo yote yenye madini ya uran katika mto mkuju wilayani Namtumbo jana.
Mjalojia mkuu wa kampuni ya Mantra Tanzani ltd,Emanuel Nyamsika akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu kipande mojawapo cha madini ya uran yaliyogundulika katika pori la hifadhi ya taifa ya Selou wilaya ya namtumbo mkoni humo.
Mkuu wa utambuzi na usalama wa jeshi la kujenga taifa (jkt) luten kanal Malembo akitoa salamu za mkuu wa JKT,Meja Jeneral Samuel Kitundu wakati wa kufunga mafunzo ya kijeshi ya miezi sita kwa vijana waliojiunga na jeshi Hilo kikosi cha 842 KJ mlale JKT hivi karibuni,katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Songea,Roy Thomas Sabaya na kushoto ni Mkuu wa Brigedi ya 401KV,Kanal John Marwa Chacha.
Afisa Mahusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania,Bernad Mihayo (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma walipotembelea katika mgodi wa madini ya uran juzi,kwa ajili ya kuona shughuli zinazofanyika katika mgodi huo.
Baadhi ya watendaji wa kampuni ya mantra tanzania ltd inayojishughulisha na utafiti wa madini ya uran katika mto mkuju wilaya ya namtumbo Mkoani Ruvuma,Emanuel Nyamsika kulia,Bernad Mihayo,wa pili kutoka kulia na afisa mazingira wa kampuni hiyo Johnnie Ntukura wa kwanza kushoto wakimuongoza mkuu wa mkoa wa Ruvuma wa tatu kulia mwenye kaunda suti kuangalia maeneo yaliyogundulika kuwa na madini ya uran katika mto mkuju wilayani namtumbo jana, wa pili kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo savery maketta.
Luten Jackson Otaite wa kikosi cha 842kj mlale jkt akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw Said Mwambungu kikosini hapo kwa ajili ya kufunga mafunzo ya kijeshi ya miezi sita kwa vijana zaidi ya 822.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw Said Mwambungu, akisalimiana na mkuu wa utambuzi na usalama wa jeshi la kujenga taifa makao makuu luten kanal Malembo katika ofisi za kikosi cha 842kj mlale jkt mkoani humo,katikati ni mkuu wa brigedi ya 401 KV John Marwa Chacha.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.
Posted by MROKI On Monday, January 23, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo