Nafasi Ya Matangazo

January 16, 2012


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) leo wamezindua rasmi mchakato wa kuwatafuta na kuwa tunza wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri kupitia kazi zao za Muziki kwa mwaka wa 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam meneja wa bia ya Kilimanjaro bwana George Kavishe alisema Mwaka jana Tunzo hizi za Muziki nchini Tanzania zilifanyiwa mabadiliko makubwa ambayo kwa mwaka huu yataendelezwa na kuboreshwa zaidi. Ambapo Mchakato wa kuwapata vinara hao utapitia hatua kuu zifuatazo:

1. ACADEMY:
ACADEMY ya Tunzo za Muziki Tanzania ni mkusanyiko wa wadau wa muziki kati ya hamsini hadi mia moja( 50 mpaka 100)kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambao huwekwa pamoja katika eneo moja kuwawezesha kuchanganua na hatimae kupata wateule (Nominees) wa kinyang’anyiro hicho baada ya majaji kujiridhisha kuwa washiriki waliopendekezwa wamekizi vigezo vyote muhimu ambapo zoezi hili kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Jan 2012.

2. Majaji:
Hatua ya pili ni Majaji ambapo huwa ni hatua muhimu sana ambapo majaji huwa na kazi moja kubwa ya kupiga kura wakizingatia vigezo muhimu vya kiufundi zaidi na vile vile kuhakiki uteuzi wa washiriki uliofanywa katika hatua ya awali kwenye Academy husika ikiwa ni pamoja na kura zitakazopigwa na wananchi. Wao hutumia zaidi vigezo halali vinavyopatikana na mkusanyiko wa rekodi za wasanii zilizotoka kwa mwaka 2011, kazi zao za mwaka 2011, Mafanikio n.k. Jopo hili hujumuisha wadau wa tasnia ya musiki kumi na tano (15).
3. KURA:
Hii ni ni hatua ya mwisho ambapo wapenzi wa musiki waliopiga kura zao Kura hizo hujumuishwa katika kuchangua washindi ambapo kwa shindano la mwaka huu kura za wapenzi na mashabiki wa wasanii zitabeba asilimia sabini (70%) na kura za majaji asilimia thelasini (30%.) na katika kufanikisha upigaji kura kutakuwa njia kuu Njia kuu nne za upigaji wa kura :
  • Njia ya ujumbe mfupi (sms).
  • Njia ya barua pepe (Email).
  • Njia ya kujaza sehemu maalum katika Magazeti.
  • Na njia ya mwisho ni njia ya vipeperushi (Fliers.)
Kwa upande wake mwakilishi wa baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Mzee Luhaja amewataka wasanii wa tasnia hiyo nchini kutumia vyema fursa ya tunzo za Kili Music Award kama sehemu ya kuweza kujitangaza katika anga za muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

Alisema msanii mzuri ni Yule anaeweza kutunga nyimbo zenye lengo la kuelimisha jamii na kuburudisha kwa kuzingatia maadili na hayo hujidhihirisha kupitia kwenye tunzo kama hizi ambazo hutoa fursa kwa wasikilizaji kutoa michango yao juu ya mwanamuziki gani aliyeweza kukonga mioyo yao kupitia tungo zake.
Posted by MROKI On Monday, January 16, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo