Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu akizindua nembo ya maadhimisho ya miaka 30 tangun kuanzishwa kwa Kiwanda cha Tanelek cha mjini Arusha. Wengine ni viongozi wa Tanelek na wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Tanelek kwa Ian Robertson ( Kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu( Wa pili toka kushoto) alipokuwa akitembelea Karakana ya Kiwanda hicho mjini Arusha. Wengine ni wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 30 ya Kiwanda hicho.
Baadhi ya wanyakazi wa Tanelek wakiwa kazini katika Karakana zao mjini Arusha.
Baadhi ya wanyakazi wa Tanelek wakiwa kazini katika Karakana zao mjini Arusha.
Serikali imekitaka Kiwanda cha utengenezaji wa vifaa vya umeme cha Tanelek cha mjini Arusha, kutumia vyema fursa za masoko zilizopo nje ya nchi na hasa kupitia jumuia za kiuchumi za kikanda ili kuongeza tija kwa kiwanda hicho.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazatro Nyalandu alipokuwa akitoa salamu za serikali katika maadhimisho ya miaka thelathini tangu kuanzishwa kwa Kiwanda hicho.
“ Ninawapongeza sana kwa kazi nzuri ya kuzalisha bidhaa bora zinazoitangaza vyema nchi yetu nje ya mipaka yetu.. Nawapongeza pia kwa kuwajali wafanyakazi wenu hali inayowaongezea nidhamu na moyo wa uzalendo.. Jitahidini kuongeza uzalishaji kwa ajili ya masoko mengi katika jumuia za kikanda, simamieni ubora ili sote tuendelee kufaidika na uwepo wenu”.
Akitoa salamu za wafanyakazi wa Kiwanda hicho, Mwenyekiti cha TUICO tawi la Kiwanda hicho Bw Gabriel Mkenda aeiomba serikali kupunguza kiasi cha kodi kinachotozwa katika mishahara, kuboresha mafao yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii na kuzitaka taasisi za Umma kuwa wanunuzi wa bidhaa zinazozalishwa nchini kabla ya kukimbilia bidhaa kutoka nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment