Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji
katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo.
Rais
Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mhe.
Majaliwa kuhusiana na zoezi la uokoaji na kusema:
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua
utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo. Binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu
anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanusuru ndugu zetu wengine ambao bado
wamenasa kwenye jengo hilo. Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji
na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini
bado wako hai “
Aidha,
Rais Dkt. Samia pia ameongeza kusema kuwa:
“Kwa vikosi vyetu vyote na wananchi wote
wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe
salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na nina wathamini sana. Wameonyesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi
wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea
kuwapambania ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu”
Rais
Dkt. Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote wakiwa wanateleleza
jukumu hilo kubwa na la kizalendo.
Kwa
upande mwingine, Rais Dkt. Samia amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea
kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu
ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa.
Mwenyezi
Mungu tunakuomba utufanyie wepesi kwenye zoezi hili. Amin
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment