Nafasi Ya Matangazo

November 18, 2011



Rais wa zanzibar Dk Ali Mohamed shein akisalimiana na makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif hamadi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar,akitokea ziarani Dubai .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na watoto baada ya kumvalisha shada la Mauwa jkana akitokea safarini katika nchi za UAE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ua kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa was Abeid Amani Karume Air Port,akitokea nchi za UAE,katika ziara za kuimarisha uhusiano wa kihistoria na nchi hizo.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kufukia eneo la Bahari kwa lengo la kuongeza Ardhi kwa ajili ya makaazi ili kupunguza ujenzi katika maeneo ya kilimo.
 
Hayo yameelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein wakatia akizungumza na Waandishi wa Habari hapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar mara baada ya kurejea ziara yake katika nchi za Falme za kiarabu hivi leo. 

Amesema tayari ameshazungumza na kiongozi wa Nchi ya Sharjah Sheikh Kasim juu ya kupatiwa wataalam wakuja kuangalia uwezekano wa ujenzi huo.
 
Amesema Sharjah imeshafanya kazi hiyo kwa ufanisi na kufanikiwa kujenga nyumba za makaazi katika maeneo ambayo yalikuwa ya bahari hapo awali.
 
Aidha amesema Nchi kama Uholanzi na nyigi nyenginezo zimeshafukia bahari na kujengwa miji ya kisasa kabisa bila ya tatizo lolote.
 
Hivyo alisema Zanzibar inayo maeneo ambayo yakifukiwa yataweza kujengwa nyumba nyingi za maendeleo kwani miaka ya nyuma kazi hiyo ilifanywa katika maeneo ya Funguni hadi Makumbusho ambalo eneo lote hilo lilikuwa Bahari.
 
Akizungumzia suala Uwekezaji Dk Shein alisema wakati umefika kwa Zanzibar kupata maendeleo ya haraka kwa kukaribisha wawekezaji wa uhakika katika Nyanja mbali mbali ili kuweza kuongeza pato la taifa.

Amesema kuwa katika mazungumzo yake na viongozi wa Sharjah na Ras Al khaima wameonyesh hamu ya kuendeleza maeneo hayo ili yaweze kuchangia katika uchumi wa Zanzibar.

Kuhusu suala la Maji safi na salama amesema Serikali ya Sharjah italeta wataalaam wa kuangalia vianzio vipya vya maji kwani utafiti uliofanywa umeonyesha kwamba maji katika visiwa vya Zanzibar yamepungua hivyo ipo haja ya kutafuta vianzio vipya kuweza kukabiliana na tatizo hilo.

Akizungumzia juu ya mafunzo kwa vijana wa Zanzibar Dk. Shein amesema kuwa Sharjah na Ras Al khaima wamekubali kuwapokea vijana wa zanzibar katika Vyuo vyao mbalimbali ikiwemo masomo ya Udaktari.

Amewaomba Viongozi wa Chuo kikuu cha Sharjah kuja Zanzibar kutembelea Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuona nyanja gani za mafunzo ambazo wataweza kushirikiana.
Posted by MROKI On Friday, November 18, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo