Shirika la ndege la Precision wakishirikiana na shirika la ndege la Kenya Airways wanayofaraja kutangaza udhamini wao katika umoja wa Gofu (TGU) ikiwa imeandaliwa na Gymkhana Club mjini Arusha ikifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Desemba 2011 jijini Arusha.
Akiongea wakati wa mkutanao na waandishi wa habari katika klabu,,Mkurugenzi wa Biashara wa shirika la ndege la Precision Mr. Phil Mwakitawa alisema kwamba mashindano ambayo yamedhamiria kukusanya wahiriki zaidi ya 100 mpaka 150 kutoka Nairobi, Arusha na Dar es Salaam ni nafasi nzuri kwa washirika wa kampuni zote mbili za ndege kujihusisha katika kutangaza uboreshaji wa afya kwa njia ya michezo ya gofu.
Na wakati huo huo Meneja wa nchi ya Tanzania wa Shirika la ndege la Kenya Airways Bi. Lucy Malu aliongeza kwamba shirika la ndege la Kenya na Precision Air waliwahi kuunga mkono hapo awali na pia wanayofaraja ya kuendelea kuunga mkono hata kwa mwaka huu kwasababu ni sehemu ya kutangaza gofu ya ubora kwa Afrika Mashariki nzima.
Mwenyekiti wa Umoja wa Gofu Tanzania , Bwana. Paul Matthysen ameomba udhamini katika shirika la ndege la Precision na Kenya Airways’ kwenye mashindano haya kama njia ya kuchangia katika kutangaza Gofu Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
“Mchezo wa Gofu Tanzania na Afrika Mashariki bado ni mchezo unaaokua. Kwa kupitia mashindano kamahaya ndipo tunapata uzoefu na kuwa katika nafasi ya juu duniani katika mchezo,” Alisema huku akisisitizia watu waje kushuhudia Mchezo huu utakaofanyika pale Gymkhana Arusha.
Shirika la ndege la Precision na Kenya Airways wametia saini katika mkataba wa makubaliano ya udhamini na Klabu ya Gymkhana Arusha kama wadhamini wakuu wa mashinano haya kwa mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment