Nafasi Ya Matangazo

November 08, 2011

Tanganyika ilipata Uhuru Mnamo mwaka 1961, ilipofika mwaka 1962 Tanganyika ikawa ni Jamhuri ya Tanganyika na mwaka mmoja baadae Kisiwa jirani na Tanganyika ambacho ni Zanzibar kilipata Uhuru wake na hii ilikuwa ni mwaka 1963. Viongozi wa Nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar kwa kutumia busara yao waliamua kuungana ili kuwa na nchi moja na wazo lao lilitimia Aprili 26,1964 pale ilipozaliwa Tanzania.
Hapo Juu ni Bendera ya Taifa Huru la Tanganyika. Bendera hii ndio ilipandishwa baada ya ile ya Utawala wa Kiingereza kushushwa 9 Desemba 1961. Leo hii Tanganyika kupitia nchi iliyozaliwa hapo baade Tanzania itaadhimisha miaka 50 ya Uhuru wake. Nini watoto wetu wa uzao huu wa sasa wanajua kuhusu hiyo nchi iliyopata Uhuru wakati huo ambayo inaitwa Tanganyika. 

Naanmakala haya mafupi kwa kuelezea kidogo historia ya Tanganyika iliopata Uhuru wake kutoka utawala wa Mwingereza. lakini uandikaji wangu umekuja ghafla ya kuona kama  kuna upotoshaji wa sherehe hizi za Miaka 50 ya Uhuru, kitu ambacho kinaniumiza kichwa na kunipa maswali mengi ambayo nikikutana na mtoto wa shule ya msingi sasa akaniuliza kuwa TANZANIA ilipata UHURU mwaka gani nikashindwa kujibu. 

Ndio kikuweli mimi sijui maana hata huo Uhuru wa Tanganyika ninaouzungumzia hapa leo nimefanya kuusoma tu katika vitabu mbalimbali vya Historia lakini hata siku moja sikuwahi kusoma sehemu iliyoandikwa UHURU WA TANZANIA kama ipo basi ni katika madarasa ya juu Chuo Kiuu ambako siku wahi ingia madara yake na hata kugusa hicho kitabu au kukiona katika maktaba.

Tena upotoshaji huu ukiwa unapiga hatua ya mbali zaidi ni pale tunapoambiwa kuwa ni UHURU WA TANZANIA BARA, tumeanza kumezwa na dhambi ya ubinafsi na kujipendelea sisi watoto wa kwanza yaani Tanganyika na kuwasahau watoto wa pili yaani Zanzibar. 

Hivi tunashindwa nini kusheherekea kwa pamoja Uhuru wa Tanzania basi kama tumeshindwa kusheherekea Uhuru wa Tanganyika amba hata wao Zanzibar wakiona tunapakua pilau la miaka 50 waseme tu bila kinyongo kuwa sherehe hiyo haituhusu maana hatujachanga ingawa sina hakika kama tutwaalika. 

Hizo logo zenu za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara ndio zimenisukuma zaidi na kunitumbuka nyongo ya mimi kuchangia gharama za pilau hili la Uhuru.

Yaani na sema kuchangia kwa maana ya kupiga makofi ya furaha kusherehekea Uhuru wa Tanzania Bara. Nitawezaje kushangilia Uhuru ambao sikuwahi soma katika Historia ya nchi ya Tanzania kuwa ilipata Uhuru kutoka kwa Wapare au Waluguru. 

Ama ni kuto kuelewa kwangu vyema Historia ya nchi hii ambayo ilizanza enzi za Ukoloni wa Mjerumani na baade kuja kwa Mwingereza ambaye wazee wangu walishirikiana na Mwalimu wa shule ya Sekondari Pugu, Hayati Baba wa Taifa la Tanzania, Julius Kambarage Nyerere kumwondoa Muingereza huyo na kupandisha bendera huru ya Tanganyika.

Unaeijua vyema Historia ya Tanganyika utajua fika Tanganyika iliwahi kutawaliwa na Marais wawili ambao ni  Rais Elizabeth wa pili aliyekuwa mtawala mwaka 1961-1962 wakati huo Nyerere akiwa ni Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na baadae mwaka 1962 hadi 1964 ndipo Nyerere alikuwa Rais hata akashirikiana kimazungumzo na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume kuungana na kuwa taifa moja lenye nguvu yaani Tanzania.
Pia tutamklumbuka Gavana Richard Gordon Turnbull aliyeshusha bendera ya Uingereza katika ardhi ya Tanganyika na kuruhusu Nyerere kupandisha Bendera ya Mtanganyika.

 Wakati ule wa Utawala wa Mwingereza katika eneo la Tanganyika alitumia Bendera hiyo hapo juu ambayo ilikuwa ikijulikana kama "Flag of the Tanganyika Territory" nadhani ndipo Twiga tulipomtoa katika kuitambulisha nchi hii kuwa Twiga ndio alama ya Tanzania.
Bendera hii sasa ikazaliwa baada ya Muungano wa Nchi Mbili jirani yaani Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa Tanzania na Zanzibar ambazo baada ya muda kidogo zikajulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rangi moja ikaongezeka kuashiria bahari tulionayo.

Leo hii tunaposema Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara sijui inatoka wapi kulingana tu na historia yangu ya vyuma chakavu. 

Mbaya zaidi tumelisahau jina la Tanganyika na kushindwa kuliebnzi jina hilo lililotupatia Uhuru japo kuna Ziwa ambalo lilikuwa likiitwa hivyo tangu enzi ya ukoloni na sio sisi ambao tumelipa jina hilo. 

Shukrani zangu ziende katika Kijiji cha Tanganyika kilichopo Wilaya ya Muheza kama sijakosea Mkoani Tanga ambao wao waliamua kijiji hicho kukipa jina hilo. Ipo haya basi hata Mkoa mmoja kati ya mikoa mipya inayokuja mwaka hadi mwaka au Wilaya mpya moja wapo kupewa jina la Tanganyika achilia mbali barabara au majengo. 

Pia nawashukuru wale wanasheria walioamua kusajili chama chao kwa jina la Tanganyika Low Society. 
Lakini vipi tunatumia gharama hizi katika maonesho mbalimbali ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara ambao kimsingi na ukwekli ni kuwa haupo badala ya kujenga hata wodi moja moja kila Hospitali kwaajili ya akina mama wajhawazito na watoto. Ni Bajeti mabilioni mangapi yametumika huku akina mama hao wakilala chini mahospitalini au watatu watatu kitandaani.
Posted by MROKI On Tuesday, November 08, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo