Nafasi Ya Matangazo

November 14, 2011

Image
 MLIMA Kilimanjaro uliopo nchini Tanzanua na ambao ni mrefu kupita yote barani Afrika, umetupwa nje ya orodha ya Maajabu Saba mapya ya dunia yaliyotangazwa juzi usiku.  
 
Taarfia hiyo ilitolewa juzi na Eamonn Fitzgerald ambaye ni msemaji wa ‘New Seven Wonders’ taasisi iliyokuwa ikiratibu upigaji kura kwa vivutio vipatavyo 28 dunia nzima, vilivyoingia fainali za ‘Maajabu Saba Mapya ya Asili.
 
Fitzgerald alibainisha upigaji hafifu wa kura kutoka Tanzania ulishindwa kuupa nguvu mlima Kilimanjaro ambao hata hivyo ulikuwa ukikusanya mamilioni ya kura kutoka nchi zingine za Ulaya na Amerika kwa zaidi ya asilimia 95. Fitzgerald ameutaja ‘Mlima Meza’ (Table Mountain) ulioko katika Jiji la Cape Town, Afrika Kusini kuwa miongoni mwa maajabu saba mapya ya dunia. 
 
 Mlima Meza na Kilimanjaro ndivyo vilivyokuwa vivutio pekee kutoka barani Afrika vilivyofanikiwa kuingia kwenye fainali ya mbio hizo za kimataifa. 
 
  Hivi sasa maajabu mapya saba ya asili ya Dunia ni pamoja na msitu mnene wa mvua wa Amazon ulioko Amerika ya Kusini, Maporomoko ya Iguazu yaliyoko Argentina, Kisiwa cha Jeju kilichopo Korea Kusini, Mto wa Chini ya ardhi ujulikanao kama ‘Puerto Princesa’ ambao uko Ufilipino na Mlima Meza (Table Mountain) wa Afrika Kusini.
Posted by MROKI On Monday, November 14, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo