Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiangalia moderm ya intaenti ya kampuni ya Vodacom wakati Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo Salum Mwalim akimpatia maelezo ya moderm hizo,wakati Waziri Mkuu alipotembelea banda la Vodacom katika maonesho ya bidhaa na huduma pembezoni mwa mkutano wa wadau wa uwekezaji eneo la ziwa Tanganyika unaofanyika Mjini Mpanda. Mkutano huo utafunguliwa kesho 17 Oktoba, 2011 na Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua madini yanayochimbwa Mpanda wakati alipotembelea banda la TPM MINING COMPANY LIMITED katika maonyesho yatakayoambatana na uzinduzi wa mkutano wa uwekezaji unaotarajiwa kufunhuliwa na Rais Jakaya Kikwete Mjini Mpanda October 17,2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Mpanda baada ya kukagua maandalizi ya mkutano wa Uwekezaji unaotarajiwa kufunguliwa na Rais Kikwete Mjini Mpanda October 17,2011. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya.
0 comments:
Post a Comment