Wakati taifa likiadhimisha miaka 50 ya Uhuru kwa kujivunia mambo mbali mbali ya maeneleo na hivi sasaWizara kadhaa zinaendelea na Maadhimisho hayo kila moja likionesha hatua mbalimbali ambazo zinapigwa na wizara husika. Nadhani miongoni mwa vitu ambavyo Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi inaweza jivunia kwa kuvifanya katika kipindi hiki ni Uhamasishaji wa Ujenzi waVituo vya Polisi nchini Kopte uliowahi kufanywa na liyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani miaka ya 90, Augustino Lyatonga Mrema.
Pichani ni moja ya vituo hivyo cha Kikundi kilichopo Manispaa ya Morogoro kilichozinduliwa na Waziri huyo 6-10-1992 na hivi sasa kimebaki gofu na haijulikani kwanini Jeshi hilo kimekifunga.
Wahalifu bilashaka wanafurahia kutokufanya kazi kwa kituo hiki ambacho kilijengwa kwa makusudi hayo ya kudhibiti uhalifu.
0 comments:
Post a Comment