Nafasi Ya Matangazo

October 10, 2011

Kulia ni Meneja wa kanda ya kusini  wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel,  Fredrick Mwakitwange akimkabithi bwana Geoff fox  (shoto) moja ya cherehani kati ya vyerehani 10 vilivootolewa msaada kwaajili ya kituo cha kulea na kusomesha watoto yatima  kinachojulikana kama Mufindi Orphans(Fox farm) kilichopo Iringa. kituo hiki kinatunza watoto 56 na kusaidia zaidi ya watoto 1200 wa vijiji vya jirani,  nyuma yao ni  baadhi ya watoto wa kituo hicho,wafanyakazi wa Airtel na wafanyakazi wa kituo hicho wakishuhudia makabithiano hayo. Mwishoni mwa wiki.
******************************************************

 Octoba 9,2011, Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imetoa msaada wa vyerehani kumi  kwa kikundi  kinacholea watoto yatima mkoni Iringa ili kukiongezea uwezo wa kupambana na changamoto zinazokikumba.
Msaada huo umekabidhiwa na meneja wa Kanda ya Kusini wa airtel Fredrick Mwakitwange kwa kikundi hicho kinacholea na kufundisha watoto yatima Iringa kijulikanacho kama Mufindi Orphans (Fox farm) chenye watoto 56 ndani ya kituo pamoja na kufundisha zaidi ya watoto 1200 wa vijiji vya jirani.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja wa Kanda ya Kusini wa Airtel Bw Fredriki Mwakitwange alisema “AIRTEL tutaendelea kugawa  misaada kwa vikundi vya wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kampeni yatu ya kusaidia jamii katika kutatua baadhi ya matatizo ambayo yanayakabili”.
Airtel tunaguswa sana na matatizo yanayowakabili watu mbali mbali katika jamii ikiwa ni pamoja na matatizo ya MUFINDI Orphans (Fox Farm) na tunaamini mashine hizi zitawasaidia kuanzisha mradi endelevu ambao utawasaidia kujitengenezea kipato ambacho kitawasaidia w watoto hawa kuweza kupata chakula, malazi, mavazi pamoja na elimu.
Airtel kwa kutambua umuhimu wa kusaidia jamii Misaada yetu bado tutaendelea kuielekeza kwenye sekta za Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii  kama tunavyofanya leo hapa Iringa.
Akipokea msaada huo wa mashine za kushonea, Mlezi wa  kikundi cha Mufindi Orphans, Kituo cha  kulelea watoto yatima Bw Geoff Fox alisema  “ Msaada huu  utatusaidia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto hawa. tunachangamoto nyingi ikiwemo idadi kubwa ya watoto na kipato kidogo cha uendeshaji, hivyo tunawapongeza sana Airtel kwa kushirikiana nasi katika kusaidia jamii.
kupitia cherehani hizi tutaanzisha madarasa ya ushonaji na ada zitakazolipwa zitatumika kusaidia watoto hawa, vilevile chereharani zitatumika kushona vitambaa na mashuka ambayo yatatumiwa na watoto pia yataleta pato katika kikundi na tutaweza hata kuendelea kuwasomesha watoto hawa vizuri” aliendelea kusema Bw Geoff Fox.
Airtel imekuwa mstari katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa   kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.Mwezi uliopita licha ya kutoa misaada ya vitabu kwa shule za sekondari mikoa ya Tanga, Moshi na Arusha pia ilitoa msaada wa cherehani 10 kwa vikundi vitatu vya kulea watoto yatima  jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kikundi cha wanawake cha Msasani,kikundi cha Huruma cha Kawe pamoja na kile cha kulea watoto yatima cha Kinondoni.
Watoto wanaolelewa katika vituo hivyo vya Dar es salaam na Iringa cha Mufindi Fox  bado wanamahitaji mengi japo kampuni ya simu za mkononi airtel imeweza kujitolea msaada huo wa vyerehani bado pia wanahitaji ya vifaa vya shule, vifaa vya kujifunzia, chakula pamoja na malazi ya kila siku.
Posted by MROKI On Monday, October 10, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo