Nafasi Ya Matangazo

October 17, 2011

  • Airtel yafanya tamasha ya miaka 50 kusherehekia uzinduzi wa huduma za wa Mawasiliano vijiji 20 Nyanda za Kusini
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imefanya tamasha la wazi mkoani mbeya lilolojumuisha wasanii mahiri  akiwemo Juma nature na kundi lake la  wanaume halisi ili  kusherehekia miaka 50 ya uhuru pamoja na uzinduzi wa huduma za mawasilino ya simu za mkononi katika vijiji 20 vya Nyanda za Kusini.

Vijiji vilivyofaidika na huduma za mawasiliano  ni Kaulolo, Nsenkwa,Mtakuja,Inyonga na Kamsisi mkoani Rukwa kwa Mkoa wa mbeya ni vijiji vya OldVwawa,Isangu,Ilolo,Ilembo,Mwantengo,Hasamba,Ukingani  Majengo, Mpangala,Kinyika,Ndapo,Nhungu,Matamba na Mahanji  wakati Mkoani Iringa ni Kibena, Tea estate.

Tamasha hilo la aina yake lililowavutia maelfu ya wakazi wa Mbeya  lilifanyika katika viwanja vya Rwandanzove ambapo msanii wa kwanza kupanda jukwaani na kuburudisha alikuwa ni  mkali wa Zuku na R&B Barnaba boy ambaye aliburudisha sana watu na vibao vyake vikali lakini ilikuwa shangwe pale alipoachia bembeleza na natumaini

Mara baada ya burudani hiyo alipanda mchekeshaji maarufu King Majuto na kutoa burudani ambayo ilienda sambamba na wananchi kusajili namba zao mara tu wanapohamia Airtel.

Burudani ya shangwe za uhuru wa kuongea kwa kuhamia airtel ilinoga baada ya jukwaa kuvamiwa na mkali wa miondoko ya bongo flava Juma Nature na wanaume halisi na kuachia vibao vinavyobamba katika burudani ikiwa ni kama” mtoto iddi”mega mixing ya yaleo kali, ah wapi, party la kijanja 770, hiligame, na hakuna kulala pia hayo Jumanature alipanga mashairi yanayoelezea  juu ya miaka 50 ya uhuru ambayo yalileta amasha na mwamko kwa wakazi wa mbeya.

Mwisho jukwaa lilimalizwa na mwanaharakati msanii wa hip pop Roma ambaye alimwaga mashairi yaliojaa vina vyakuwapa wananchi wa mbeya matumaini na pole kwa wale wanaopigwa nondo na watu wasiojulikana kwa mambo yanayosemekana ni yakishirikina yalioanza hivi karibuni huko mbeya.

Poleni watu wambeya mnaopigwa nondo kwa imani za kishirikina ili watu wauze mabucha…. Yaliseme baadhi ya mashairi ya msanii huyo.

Pia aliwaomba wananchi wote waliojaa kiwanjani hapo kuinamisha kichwa chini kwa sekunde chache kama ishara ya kumuenzi baba wa taifa na kasha akaanza na kibao chake cha mr president, na kuendelea na pastor, Tanzania, mechi za ugenine na kumaliza na nyimbo iliyozua gumzo zaidi ya mathematics.

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alifunga burudani hizo kwa kusema “Airtel inaendelea kupanua mtandao na kuwapatia wateja wake huduma bora kwa kuwafikia wananchi wengi na kuboresha huduma hasa katika vijiji mbalimbali nchini.
“Mkakati wetu wa kupanua mawasiliano vijijini unaendelea kwa kipindi chote cha Mwaka huu lengo letu ni kuhakikisha tunawafikishia wananchi wote huduma ya mawasiliano yenye utulivu zaidi kutatoa uhuru wa mawasiliano zaidi  kwa wateja  kuendelea kufanya mawasiliano yenye manufaa yatakaowafanya wafurahie kutimiza miaka 50 ya uhuru wakiwa na miundombinu ya mwasiliano yanayojitosheleza.
Posted by MROKI On Monday, October 17, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo