SIKU chache baada ya Waziri mkuu Mizengo Pinda kusema Polisi nchini wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kazi kutokana na kuruhusu uvushwaji wa sukari nje ya nchi, ili kupisha jeshi la kujenga taifa JWTZ kufanya shughuli hiyo, Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kukamata mifuko 2,074 ya sukari iliyokuwa kisafirishwa
kwenda nchi jirani ya Kenya.
Akizungumzia kukamatwa kwa sukari hiyo katika eneo la tukio, kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Absalum Mwakyoma, alisema kuwa sukari hiyo ilikamatwa Septemba 26 majira ya saa kumi na moja jioni katika eneo la mji mdogo wa Himo wilaya ya Moshi Vijijini.
Kamanda Mwakyoma alisema kuwa mifuko hiyo ilikamatwa ikiwa imepakiwa kwenye magari tofauti na nyingine ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala, ambapo alisema gari lenye namba za usajili T960 AAV aina ya Fuso ikiwa na mifuko ya sukari 230, linguine ni T508 AXY aina ya Fuso likiwa na mifuko 320.

Habarizaidi Gonga hapa.
0 comments:
Post a Comment