Nafasi Ya Matangazo

September 11, 2011

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Haji Duni (kushoto) akipokea  msaada wa vyakula, dawa, maji na misaada mingine ya kibinadamu  iliyotolewa na Benki ya NBC kutoka kwa Meneja wa Tawi la benki
 hiyoVisiwani Zanzibar, Rajab Maalim kwa ajili ya wahanga wa ajali ya  Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani  humo.. Hafla ilifanyika Zanzibar juzi.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Haji Duni (katikati) akizungumza  baada ya kupokea msaada wa vyakula, dawa, maji na misaada mingine ya  kibinadamu iliyotolewa na Benki ya NBC kwa ajili ya wahanga wa ajali  ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani  humo. Katikati ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja  na nyuma ya Masanja ni Ofisa Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina. 
 Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Rajab Maalim (kulia)  akizungumza katika hafla ambayo NBC ilikabidhi  msaada wa vyakula,  dawa, maji na misaada mingine ya kibinadamu iliyotolewa na benki hiyo  kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea  usiku wa Septemba 10 visiwani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika  visiwani humo mwishoni mwa wiki. Katikati ni Waziri wa Afya wa  Zanzibar, Juma Haji Duni na wa pili kushoto ni Mshauri  wa Mambo ya  Habari wa NBC, Redemptus Masanja.
Ofisa Uhusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina (wa pili kushoto)  akisaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wakazi wa  Zanzibar kushusha baadhi  ya vitu vilivyotolewa msaada na benki hiyo  kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea  usiku wa Septemba 10 visiwani humo. Hafla ya makabidhiano  ilifanyika  Visiwani Zanzibar jana.
Posted by MROKI On Sunday, September 11, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo