Nafasi Ya Matangazo

September 16, 2011

Wakati taifa likiadhimisha miaka 50 ya Uhuru baadhi ya huduma muhimu za Jamiii zimezidi kuwambaya licha ya kujivunia kuzisambaza kwa wingi. Miongoni mwa huduma hizo ni za Afya ambapokatika Hospitali nyingi za Mikoana Wilaya Wanawake wajawazito na baadhi ya wagonjwa wamekuwawakilazwa wawili wawili au zaidi vitandanani kama hawa hapa pichani wa  wodi namba mbili katika hospitali ya wazazi Meta jijini Mbeya kufuatia uhaba wa majengo unaosababisha kukosekana kwa mahali pa kuweka vitanda kama walivyokutwa jana.Wodi hiyo yenye uwezo wa kulaza mama wajawazito 32 inalazimika kulaza wajawazito 74 kwa wakati mmoja.
Posted by MROKI On Friday, September 16, 2011 2 comments

2 comments:

  1. Lamuhimu hapa,kuhusu tatizo hili,ni kufanya harambee,kwa watu wa eneo hilo,hasa mkoa wa mbeya,kuna wafanya biashara wengi tu,na baadhi ya watu wenye uwezo wao,tafuta namna watu watakutana nakufanya hiyo harambee.baada ya hapo iambieni srikali na watendaji wake wa hakikisha mahitaji muhimu, yana patikana ikiwemo madaktari wa kutosha ambao nijukumu la serilkali kuwalipa mshahara.pia hojini bajeti ya serikali katika mkoa wa mbeya,hasa kwa upande wa afya.unaweza kukuta pesa zipo ila ufuatiliaji hakuna.nahii ndo kazi ya wabunge.wananchi tukishrikiana kwa pamoja na kuweka siasa pembeni,kwa kuwauliza hawa watendaji kuhusu huduma zao mtagundua mengi.inasikitisha sana miaka 50 bado tu ubabaishaji. kaka S

    ReplyDelete
  2. USHAURI ULIOTOA MDAU UNAONEKANA HUELEWI HALI HALISI, TUNAONGELEA RAISI KUJIUZULU!!! UNAONGELEA HARAMBEE!! AU NI KWASABABU HUBEBI MIMBA?!!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo