MASHINDANO YA MASHUA YA JOHNNIE WALKER THE LASER OPEN COMPETITION YAMALIZIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Mwendesha mashua bora wa Afrika Mashariki Al Bush akipokea kikombe chake cha ushindi kutoka kwa Benjamin Mariki Meneja wa vinywaji vikali kutoka kampuni ya Serengeti Breweriers (SBL), mara baada ya kuwashinda waendesha mashua wenzake kutoka nchi 15 katika mashindano ya Johnnie Walker THE LASER OPEN COMPETITION yaliyoanza juzi na kumalizika leo kwenye klabu ya Dar es salaam Yacht Club (DYC) Masaki jijini Dar es salaam. Mwendeshaji huyo wa mashua Bw. Al Bush amesema amekuwa akiendesha mashua kwa muda wa miaka 25 sasa na amekuwa mshindi katika mashindano hayo kwa miaka 9 katika mashindano yaliyofanyika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki. Katika picha kulia ni anayeshuhudia ni Hellen Rattansi Meneja Mauzi na Masoko. Kampuni ya bia ya Serengeti Breweriers SBL ndiyo iliyodhamini mashindano kupitia vinvywaji vyake vikali vya John Walker na yaliomalizika leo jijini Dar es salaam









0 comments:
Post a Comment