Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi wa Precision Air Bw. Michael Shirima akizungumza na hadhara ya abiria wa kwanza wa safari ya Precision Air kwenda Johannesburg katika kumbi ya VIP uwanja wa kimataifa Julius Nyerere. Bw. Shirima alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wateja na wadau wote wa Precision Air kwa ushirikiano mkubwa walionyesha kuweza kufanikisha safari hizo. “Hakika hii ni hatua kubwa sana lakini najua bila nyinyi tusingeweza kufika hapa, kwahiyo napenda kuwapongeza wateja wetu na wafanyakazi wote wa Precision Air kwa kazi nzuri. Nategemea mtafaidika kibiashara na kitalii kwa safari hizi,” alisema. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga nchini Tanzania (TCAA) Bw. John Njawa. Hi ndivyo hali ilivyokuwa ndani ya ndege hiyo iliyofanya safari ya saa 4 kwenda Johannesburg, ilibeba ya abiria 111, jumla ndege hiyo inauwezo wakubeba abiria 116.Wadau wa Precision Air wakifurahia huduma za Business Class kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini ndani ya Boeing 737-300.Mdau Amani Nkurlu Afisa Mawasiliano wa Precision Air akiwa na mwanahabari mkongwe Jenerali Ulimwengu katika hafla fupi ya mapokezi yaliyofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oliver Tambo, Johannesburg nchini Afrika Kusini. Msafara maalumu wa Precision Air ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko upo Jo’Burg nchini Afrika Kusini kwa uzinduzi na ziara maalumu itakayochukua takribani ya siku mbili. Wadau mbali mbali wenyeji wa Afrika Kusini na Tanzania wote walihudhuria hafla hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa O. Tambo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment