Nafasi Ya Matangazo

August 26, 2011

Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akiwakaribisha wadau na waandishi wa habari katika semina hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania nchini,  juu ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) Semina imefanyika kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Ukuaji Uchumi kutoka FAO Dkt. Vedasto Rutachokozibwa akibadilishana mawazo na waandishi wa habari katika Semina ya UNDAP iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa watumishi wa IAGG Bi. Salome Anyeti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya masuala ya Haki na Jinsia katika mwendelezo wa semina iliyoandaliwa na UN Tanzania kwa lengo la kuhamasisha waaandishi wa habari kuandika na kuelimisha jamii juu ya mpango wa MKUKUTA  na MKUZA  kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Kushoto ni Bw. Robert Basil Mwenyekiti wa IAGG upande wa Jinsia na Maambukizo ya Ukimwi kutoka kitengo cha Chakula na Kilimo UN.
Waliokaa Kushoto ni Afisa Mipango wa Taifa (Elimu) kutoka UNESCO Godfrey Mnubi na anayefuata Bi. Maria Westergren wa UNESCO wakitoa ufafanuzi juu ya Mpango wa miaka 4 ya UNDAP kwa upande wa Sekta ya Elimu.
Afisa Program wa WFP Said Johari na Afisa Uhusiano wa michango wa WFP Fizza Moloo wakizungumza na mwandishi wa habari alitembelea kitengo hicho wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assitance Plan 2011-2015 (UNDAP).
Posted by MROKI On Friday, August 26, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo