WANYANGE wanao wania Mataji ya Kanda za Redd’s Miss Ilala, Kinondoni na Temeke keshokutwa watashiriki michezo mbalimbali na waandishi wa habari wanawake itakayofanyika katika ufukwe wa Mbalamwezi.
Michezo hiyo itakuwa ni kuvuta kamba, kukimbia, kukimbia na gunia, kuimba na soka ambapo lengo kubwa ni kuwaweka warembo hao karibu na wanahabari ili kuwapa fursa ya kuuliza maswali na masuala mengine muhimu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Fimbo Butallah alisema kuwa anatambua mchango wa vyombo vya habari katika kuendeleza shughuli za warembo.
Alisema kuwa kupitia michuano hiyo warembo watapata fursa ya kuwa pamoja na warembo wa kanda nyingine mbalimbali na kuona upinzani wa urembo ulivyo.
Aliongeza kuwa Redd’s ikiwa kama kinywaji cha warembo kina mkakati wa kuwafikia wanawake wote kwa namna tofautitofauti kupitia urembo, michezo na shughuli nyingine muhimu.
“Ni kwamba wanahabari kwa ujumla ni wadau wetu wa TBL na huu udau upo kupitia bia zetu mbalimbali na kwa kuwa Redd’s ni kinywaji cha akina dada, sasa huu ni wakati kwa wanahabari akina dada kuwa karibu na washiriki wa michuano hii ya Redd’s Miss na kuendelea kuwa pamoja,” alisema Butallah.
Naye mratibu wa michezo hiyo kwa upande wa waandishi wa habari, Vicky Kimaro alisema kuwa michezo hiyo ni muhimu kwa kuwa inawaweka karibu waandishi wa habari wanawake na warembo na kuwafahamisha masuala mbalimbali muhimu.
Alisema kuwa waandishi hao watapata fursa ya kuwashauri, kuwakosoa na kuwaelekeza masuala muhimu yahusuyo urembo na jamii kiujumla.
Source: TSN

0 comments:
Post a Comment