Nafasi Ya Matangazo

July 25, 2011

Rais wa Jakaya Kikwete, akiwaongoza viongozi wa Kiserikali wakati wa heshima maalum kwa ajili ya kuwaombea Mashujaa waliopigana vita katika aridhi ya nchi ya Msumbiji, ambapo jumla ya miili ya askari 101 walihamishwa kutoka Msumbiji mwaka 2004 na kuzikwa katika Makaburi Naliendele mkoani Mtwara kati ya 108  waliofariki katika vita hivyo. Sherehe hizo za kuwakumbuka mashujaa hao zimefanyika leo Julai 25, 2011 katika viwanja vya makaburi hayo mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao (juu) na Upinde , katika Mnara wa Mashujaa mahala walipozikwa Mashujaa 101 waliopigana vita Msumbiji, ikiwa ni siku ya sherehe ya kuwakumbuka Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja hivyo vilivyopo Naliendele mkoani Mtwara leo Julai 25, 2011.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea kukagua makaburi 101 kati ya 108, ya askari ‘Mashujaa’ walifariki wakati wakipigana vita Msumbiji na kuzikwa katika Makaburi ya Naliendele mkoani Mtwara,

 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (mbele) na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein wakikagua makaburi hayo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Makaburi ya naliendele mkoani Mtwara.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sherehe hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimia wananchi katika sherehe hizo.
 Baadhi ya wazee waliopigana vita ambao ni moja ya mashujaa wa Tanzania waliohudhuria sherehe za mashujaa.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakitembelea Chumba cha Makumbusho cha Mashujaa kilichopo katika Viwanja hivyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee waliopigava Vita, ambao ni sehemu ya mashujaa wa Tanzania
Posted by MROKI On Monday, July 25, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo