Nafasi Ya Matangazo

July 25, 2011

Naibu waziri wa Afya na Ustawi  wa Jamii Lucy Nkya (katikati), naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri (kulia) na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole-Nangoro (kushoto) wakijadili jambo leo wakati wa kikao cha bunge la  bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika  Prof. Jummanne Maghembe akiwasoma bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Magharibi Zanzibar Mjumbe Msuri Mjumbe (wan ne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa CCM wa wilaya hiyo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
Viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) wakifuatilia kwa umakini bajeti ya wizara ya  Kilimo,  Chakula na Ushirika  wakati waziri wa wizara hiyo Jummanne Maghembe (hayupo pichani) alipokuwa akiisoma leo  bungeni mjini Dodoma. TMF kupitia mpango wao wa fellowship kwa mwaka huu imefadhili waandishi wa habari watano kwa ajili ya kuandika habari za uchunguzi kuhusu masuala ya kilimo  vijijini kwa kipindi cha miezi sita.
Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi (kushoto)  akimsikiliza Naibu waziri wa Nishati na Madini Adam Malima (kulia) mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha asubuhi cha maswali na majibu katika bunge la 10 la mkutano wa bajeti kikao cha thelathini na mbili  kinachoendelea mjini Dodoma.
Posted by MROKI On Monday, July 25, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo